Wenzetu wa upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi. Lakini uzuri watanzania wanajua uongo na leo nitawapeni ushahidi wa mambo ya uongo watu hawa wamesema.
Ukija kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege, kiwanja cha ndege hatujajenga Chato peke yake. Tunajenga Singida, Mpanda. Na kwanini tumejenga Mpanda? Juzi anasema uwanja wa ndege wa Mpanda umejaa majani, hivi kweli?
Mimi sipendi kuzungumza mambo ya mtu binafsi, nafahamu mwaka 2017 huyu bwana alipata matatizo, amatatizo wanapata watu wengi lakini nna shaka somewhere, somehow pahala fulani hivi iko shida kwenye memory.
Uwanja wa ndege wa Mpanda haukujengwa kwa sababu ya Mizengo Pinda, uwanja wa ndege wa Mpanda ambao unafanya kazi mpaka leo hii asubuhi, ndege inatua pale ya bombadier, abiria wengi wanaotumia uwanja wa ndege wa Mpanda sasa hivi ni watalii.