Polepole tulishamzoea kwamba ni mnafiki wa aina ya wale watu anayeweza hata kukana jina lake mwenyewe! Polepole yule wa Tume ya Jaji Warioba sio huyu anayeongea sasa!
Kamwe hawawezi kuiokoa CCM kwa kucheza mziki anaopiga Lissu! Hayo mambo ya Chato, SGR na vingine kila mfuatiliaji wa mambo hapa nchini anayajua na anajua dosari zake ila tu watu wapo kimya sababu wamenyimwsa uhuru wa kuongea!
Lissu sasa amekuwa sauti ya wengi walio kimya ndio kisa cha kujaza nyomi katika mikutano yake sababu anaongea masuala yanyogusa wengi! Polepole na CCM yake waje na sera za matumaini mapya kwa wanchi na sio kukariri ilani za vyama vingine!
Wakulima walishapigika, wanalima lakini soko la mazao hakuna! Vijana wanasoma huku wazazi wakijifilisi kwa kuuza ng'ombe na viwanja, lakini wakimaliza vyuo ajira hakuna!
Watumishi waliambiwa wachape kazi kufa na kupona kupitia slogani ya Hapa kazi tu, wamejikamua kuchapa kazi, lakini mishahara mipya na madaraja hakuna! Wavuvi wana mazingira magumu sana, wanashindwa kufikia bei ya vibali vya uvuvi, wameishia kukamatwa na kuchomewa nyavu badala ya kuwawezesha!
Wastaafu wanazungushwa mafao yao ambayo ni michango yao waliyo changia katika mifuko bila kuzungusha wa kuleta usumbufu wowote, Lakini leo huku mishahara yao ikiwa ilishasitishwa, bado wamekuwa watu wa nenda rudi, nenda rudi huku maisha yakiwa ni magumu sana!
Wanufaika wa Bodi ya mikopo, wanalia na marejesho ya 15% wanataka unafuu wa marejesho hayo! Waliobomolewa nyumba zao bila fidia, wengine mpaka leo hawajanunua hata viwanja, wote hawa wanaungua na ugumu wa maisha, wanataka sera zitakazowapa unafuu! Hivyo Polepole kama ana hoja ajibu kwanza haya!