Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Mwambie polepole atuoneshe proof za transactions za kibenki kati ya BOT na Boeing na Bombardier kuonesha tulilipia shilingi ngapi kwa kila ndege.

Kusema Bunge lilitenga kiasi fulani kwa kununua ndege haimaanishi kuwa hela yote ilienda kutumika kununulia ndege!!!

Bado pole pole hajajibu hoja za shujaa Lissu. Ni kweli ni Magufuli na Doto James tu ndo wanajua hizo ndege zimelipiwaje 😂😂😂😂😂
 
Haha mtaongea yote mzee na ndio zenu MTU akiwapinga basis mhamiaji haramu
Kwa taarifa yako ni kuwa wasemayo hayo hapo KASUMULU ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani, hata Kiswahili chao si unakisikia ni cha kuunga unga!
 
Mwaka huu mmekamatika bwashee nilikuwa kyela kijiji cha kasumulu sikuamini wale wazee wanasema magufuli akapumuzike kwa kweli yani maparachichi ndizi zetu tunapeleka sokoni kuuza tunaambiwa kitambulisho se se akapumzike kwa kweli hayo ni maneno ya kina bibi wa kasumulu kyela na uzuri nipo na tour ya kuzunguka kila mkoa na baadhi ya vijijini ki ukweli CCM safari hii msijidanganye vijijini huko mna hali mbaya sana kuliko hata Mimi nilivyo kuwa nikifikili kumbe watu walikuwa na yao moyoni.

Kwa sasa naelekea sumbawanga mwimbi na mambwe nimejitolea kifanya hii kazi bila kulipwa chochote na mtu
Ohoooh...😂😂,ngoja nikae kimya ,nisikuharibie usingizi wako.
 
Hilo suala la watu waliouwawa unalisema sana. Hebu toa mifano ndugu yetu ili tufahamu ukweli wako...
Inamaanaa unauliza swali Au unajijibu? Hajamuuuwa azroy gwanda? Hajamuuwa akwirina?hajamuuwa Ben sanane? Wale aliokuwa anawatupa kule baharini ni Mbuzi zako? Wale waliouwawa kibiti ni mbuzi zako? Wale wanaopotea unadhani wanaenda wapi? Unaosikia kila Siku polisi inasema kuwa imeuwa kumi, Mara Saba Mara nane, wewe Kwa akiri yako unadhani wanaposema kuwa ni majambazi unadhani ni majambazi?

Ulisikia wapi majambazi wakarushiana risasi na polisi Halafu polisi ikawauwa wote pasipo hata polosi mmoja kujeruhiwa? Ulisikia wapi? Kwa akiri yako ya kawaida ulisikia wapi? Halafu unadhani mpinzani kwenye nchi hiii anaweza mpiga mtu risasi Halafu uchunguzi uakakatazwa na wakuuu kufanyika? Ulisikia wapi? Ulisikia wapi mpinzani aue Halafu polisi wakatae kufanya uchunguzi?

Magufuli anaamulu watu wanakamatwa anawakabidhi polisi anatoa amaelekezo than wanasema ni majambazi na Kwa hali Ya ukatiri na ukiukwaji wa katiba na unyimwaji wa uhuru ndio inawapa kiburi maanaa ahakuna anaeweza kuhoji
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kupoteza muda wake wa two hours kumsikiliza mtu kama Polepole
 
Jambo La kusikitisha vyombo vyetu vya habari viko upande mmoja, muda wote ni ccm tu. Kiukweli haki imepotea sana...
 
Namsikiliza hapa,jamaa anatupa nondo kali amepangua hoja zake kwa ushahidi na kisomi sana.Sema naye kaamua kumtukana live Lissu😂.Anamuita jambazi,mnafiki,tapeli, mjinga na mtu asiyekuwa na kumbukumbu vizuri.Niliona ni Kama kamkosea heshima Ila kwa sababu alizotoa,nimekubali.
Nilimsikia Polepole akiwa na Hansard za bunge akidai Lissu amepotosha akidai ana upungufu wa kumbukumbu. Lakini amekwenda mbele zaidi kutamba kuwa siku zilizobaki CCM itaanza kuanika madudu ya wapinzani.Ngoma inogile,bado mwezi mmoja wa kugombea wapiga kura.
 
Jambo La kusikitisha vyombo vyetu vya habari viko upande mmoja, muda wote ni ccm tu. Kiukweli haki imepotea sana...
Mkuu Wala Hilo lisikukatishe tamaaa twende tukapige kura tuwaoneshe Kama siyo kusaonyesha ili wajue sisi Ni washindi
 
Nilimsikia Polepole akiwa na Hansard za bunge akidai Lissu amepotosha akidai ana upungufu wa kumbukumbu. Lakini amekwenda mbele zaidi kutamba kuwa siku zilizobaki CCM itaanza kuanika madudu ya wapinzani.Ngoma inogile,bado mwezi mmoja wa kugombea wapiga kura.
Kuna watu humu JF, wao Ni kupelekwapelekwa na huyo mgombea wa Mbowe, sisi ndo tunajua nini kinaendelea.

Tarehe 15/10, atakuwa na press nyingine itakayo mmaliza kabisa Lissu,kibaya zaidi kila wanalopanga na kujadili sirini,sisi tunalo😂, Ni mwendo wa kuwadukua tu😂😂.Kwa mikakati hiyo potofu wanayo panga, tarehe 28, watapigwa kipigo Cha mbwa mwizi
 
Back
Top Bottom