Polepole: Utaratibu wa CCM ni kuwa, Samia alitakiwa kuishia 2025 na kukabidhi kwa mwingine

Salaam!

Kuna kitu Polepole anekiongea kizito ambacho tumekuwa tukikisema humu mara nyingi.

Ameenda mbali na kudai, ikiwa tuna mashaka na akisemacho, tukamuulize Mzee Mangula!

1. Ni hivi, amesema Spika wa bunge, VP,Waziri Mkuu ni marufuku kupitishwa kuwa wagombea urais ,huo ni utaratibu ,miiko na desturi walizojiwekea wao wa ccm,ingawa ni haki yao kikatiba kugombea Urais.

2. Amedai pia kuwa, baada ya kifo Cha JPM, ilitakiwa amalizie awamu aliyoanza Magu Kisha kukabidhi kwa mwingine, huo ni utaratibu wa CCM,ingawa ni haki ya kikatiba kwa aliyepokea kijiti kugombea sawa sawa na isemavyo katiba.

Sasa alichofanya Samia ni kufumbia macho utaratibu uliopo ndani ya CCM ambao pia umemuondoa PM kugombea Ubunge kwa awamu ingine baada ya miaka 10 ya uwaziri Mkuu kwisha.

Tunakushukuru Mh Polepole kuliweka hili wazi maana hata huku kijijini kwa Hali ya kawaida, boss akifariki, ukapewa kushika Nafasi yake kwa muda, unatakiwa kukabidhi madaraka baada ya muda wa marehemu kwisha, Ili wana ukoo wamchague wamtakae, kulazimisha kuendelea ni kutengeza taswira mbaya juu ya...

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏

Haipo Siri pole pole kasema vyema sana bila hivyo wahuni wangekuwa na nafasi ya kujipenyeza.
 
Kilichompitisha mwinyi ni sababu aliwahi kuwa president wa Zanzibar,

Nionyeshe Waziri Mkuu, vp, spika aliyepitishwa Urais tangu uhuru!
Hakuna lay down procedures za Polepole theories, just hallucinations.
Anasumbuliwa na Salsa,Calypso,Lambda,Chachacha za Caribbean na Latino.
 
Salaam!

Kuna kitu Polepole anekiongea kizito ambacho tumekuwa tukikisema humu mara nyingi.

Ameenda mbali na kudai, ikiwa tuna mashaka na akisemacho, tukamuulize Mzee Mangula!

1. Ni hivi, amesema Spika wa bunge, VP,Waziri Mkuu ni marufuku kupitishwa kuwa wagombea urais ,huo ni utaratibu ,miiko na desturi walizojiwekea wao wa ccm,ingawa ni haki yao kikatiba kugombea Urais.

2. Amedai pia kuwa, baada ya kifo Cha JPM, ilitakiwa amalizie awamu aliyoanza Magu Kisha kukabidhi kwa mwingine, huo ni utaratibu wa CCM,ingawa ni haki ya kikatiba kwa aliyepokea kijiti kugombea sawa sawa na isemavyo katiba.

Sasa alichofanya Samia ni kufumbia macho utaratibu uliopo ndani ya CCM ambao pia umemuondoa PM kugombea Ubunge kwa awamu ingine baada ya miaka 10 ya uwaziri Mkuu kwisha.

Tunakushukuru Mh Polepole kuliweka hili wazi maana hata huku kijijini kwa Hali ya kawaida, boss akifariki, ukapewa kushika Nafasi yake kwa muda, unatakiwa kukabidhi madaraka baada ya muda wa marehemu kwisha, Ili wana ukoo wamchague wamtakae, kulazimisha kuendelea ni kutengeza taswira mbaya juu ya...

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏
Imemkata.
 
Katiba ya chama ikikukataa maana yake hata katiba ya mchi pia haikukubali.

Mtu anaefanya Kuinajisi katiba ya ccm na kuikanyaga katiba iyo hawezi kuiheshimu katiba ya nchi akiwa madarakani.
 
Nyerere kabla ya kukabidhiwa nchi na kuwa Raisi wa kwanza wa Tanganyika na baadae Tanzania baada ya muungano usio eleweka.

Alikuwa waziri mkuu kabla nchi haijawa Jamhuri.

Huo utamaduni wa C.C.M kama upo ulianza lini na alianzisha nani, tukumbuke mrithi wa T.A.N.U ni Sisi kwa sisi.

Anastahili kuendelea mpaka 2035
 
Kabisa na kwa nn hakushindanishwa
Anaamini msemo ule kwamba wakiwezeshwa, wanaweza.

Sasa amesahau unyeti wa Nafasi Ile, haihitaji hisia, ni UWEZO na maamuzi binafsi, SI kuuliza Kila kitu kwa mshauri Mkuu.
 
Nyerere kabla ya kukabidhiwa nchi na kuwa Raisi wa kwanza wa Tanganyika na baadae Tanzania baada ya muungano usio eleweka.

Alikuwa waziri mkuu kabla nchi haijawa Jamhuri.

Huo utamaduni wa C.C.M kama upo ulianza lini na alianzisha nani, tukumbuke mrithi wa T.A.N.U ni Sisi kwa sisi.

Anastahili kuendelea mpaka 2035
Aisee
 
Mama hata hawazi, mkitaka mabadiliko watu wawe tayari kuandamana na kupambana na polisi. Machawa wawe wanatekwa na kupotezwa kama wanaokosoa serikali.
Akili finyu ni Mzigo kwa Familiar yako.....
Nchi ya Tanzania chini ya Rais Samia imekuwa Kinara wa Amani Africa Mashariki sasa wewe unayechochea vitu vya kijinga anza kujiteka mwenyewe kama ilivyo destur yenu msingizie mnatekwa.

DIRA-3.png
 
View attachment 3410862
Mbona sijabisha kuhusu mama kushinda uchaguzi 2025 na atachukua pia 2030.Maana watanzania wanamsubiria Mungu ana watu wanaobashiri kuna anguko kubwa.
 
Atoke sasa nini kinamfanya an'gan'ganie na watu hawamtaki hili liko wazi kabisa ona msiba wa Mpoto yanayomkumba why asitumie busara tu akajifiche kwao?
 
Na kazi ya Kikwete sio kuchekacheka ahakikishe taratubu zinafuatwa,hata alambe asali aloe mdomo wote Kikwete usisahau kazi yako baada ya Philips Mangula kung'atuka.
Ili mkewe asipate fedha za uwenza na ubunge na mwanaye akose fedha za uwaziri na ubunge pia waanze kuchunguza miradi ya Miraji na Salama? No way huyu ni kadi yake ya turufu.
 
Back
Top Bottom