#COVID19 Polepole: Watanzania tuendeleeni kutumia njia za asili kupambana na Corona

#COVID19 Polepole: Watanzania tuendeleeni kutumia njia za asili kupambana na Corona

Hakuna atakae kuwa na jibu sahihi la corona hapa Tanzania kwasababu hakuna takwimu.

Watu waliokufa kwa corona kwenye nchi nyingi ni wachache na waliopona ni wengi na ambao hawakupata ni wengi zaidi.

Kwa mfano, Kama Tanzania tupo milioni 60, inawezekana waliougua ni kama milioni 5, na waliofariki labda ni laki 2. Hali kama hii sio rahisi

kuitambua na ukipita barabarani na mitaani utaona maisha yanaendelea na kuamini tupo salama.
 
Ini, figo, DNA destruction na mengine mengi.

Madalali wa chanjo hawataki kusikia hayo.

They are very vicious and money-propelled like zombies..

Daah GMOs noma

Jamaa wanataka kutubadilisha uhalisia wetu bila huruma aisee

Pata picha mapapai na maparachichi yalivyo makubwa sikuhizi mpaka unaogopa kununua sijui km TFDA wamechunguza hili aisee. Sasa kitu kinakuja kinaingia kwa damu mwilini..tutapata habari yetu sijui wanataka tuwe marobot.

Hapa ndio tutamkumbuka mkemia wetu JPM. Rest easy Baba!
 
Katibu mwenezi msitaafu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Humphrey Polepole amehoji ni kwa nini watanzania wanataka kuacha mbinu za asili zilizotusaidia mwaka jana kupambana na corona na tukaibuka na mafanikio makubwa kiuchumi na kijamii?

Bwana Polepole ametolea mfano wa nchi zote zilizojaribu kupambana na Corona kwa kufuata mfumo wa kimagharibi mwishoni wa mwaka 2020 ziliishia kupata ukuaji hasi wa uchumi kwenye nchi zao!

Polepole amesema ni Tanzania tu ndiyo iliyopata ukuaji wa uchumi chanya kwenye nchi zote za Afrika mashariki. Sasa kwa nini sisi watanzania tunaona aibu kujivunia hizo mbinu za asili? Amehoji mh Polepole.

Mwaka jana tulipambana na Corona kwa kutumia njia tatu.
1. Kumtanguliza Mungu mbele
2. Kufuata mbinu mbalimbali tunazoshauliwa na watalaamu wetu
3.Kuchapa kazi kwa bidii

Katika watu punguwani duniani huyu idiot pole pole nae yupo. Uchumi wa tz kwa sasa ni asilimia nne nukta kadhaa anasema njia za asili zimesaidia kukua kwa uchumi. Mtu kama huyu ni kirusi cha covid corea ya kusini saa hizi angeshakuwa makaa. Hawa ndiyo watu wa kupotea siyo akina ben saa nane
 
Umeshauliza uchumi wa Rwanda, Kenya ,Uganda ni asilimia ngapi?
 
Hakuna atakae kuwa na jibu sahihi la corona hapa Tanzania kwasababu hakuna takwimu.
Watu waliokufa kwa corona kwenye nchi nyingi ni wachache na waliopona ni wengi na ambao hawakupata ni wengi zaidi.
Kwa mfano,Kama Tanzania tupo milioni 60, inawezekana waliougua ni kama milioni 5, na waliofariki labda ni laki 2. Hali kama hii sio rahisi kuitambua na ukipita barabarani na mitaani utaona maisha yanaendelea na kuamini tupo salama.
Wewe wamekufa wangapi kwenu kwa corona?
 
Wewe wamekufa wangapi kwenu kwa corona?
Sina vitendea kazi vya kupima watu nijue nani ana corona na nani hana na sina mamlaka hayo, na wenye mamlaka hayo pia hawajatoa takwimu, kwahiyo sina jibu.
 
Umeshauliza uchumi wa Rwanda, Kenya ,Uganda ni asilimia ngapi?
Hakuna mahali nimeuliza swali nimetoa maoni yangu sasa wewe unayeuliza maswali tena wakati tuliambiwa tuko kwenye uchumi wa kati juzi tumeambiwa tofauti. Sasa kama uchumi unakuwa kutoka 7 kwenda 4 asilimia maana yake embe linaanguka kutoka chini kwenda kwenye mti. Baki na maswali yako kama bado uko mwanafunzi kamalizie unachosomea
 
Suala la kumtegemea Mungu katika kupambana na corona hakuepukiki. Ni ujinga na kiburi cha mwanadamu kudhani kwamba kila tatizo lipo ndani ya uwezo wa mwanadamu kusolve.

Mkuu wetu wa nchi awamu ya tano alilielewa hilo na neema ya Mungu ilitufunika na imeendelea kutufunika hadi leo hii. Wasiomwamini Mungu wapuuze tu, lakini kwetu sisi acha Mungu aitwe Mungu.
Ni kweli swali la kumtegemea Mungu hakuepukiki. Mungu ninayemjua alituweka katika uumbaji wake ili tutawale juu ya viumbe vingine - na hapo nahesabu virusi pia. Si ujinga na kiburi kujiambia "Sihitaji kutumia vipaji nilivyopewa na Mungu ili niweza kutunza familia yangu na kwuasaidia majirani yangu maana inatosha kusali" - hata kama Mungu ametuhurumia kwa kutupa akili ya kupambana na moto na umaskini na magonjwa?

Polepole alisahau katika orodha yake ya mbinu za kupambana na Covid "Kuficha habari na idadi ya vifo na kumtisha kila mtu anayesema neno Covid".
 
Katibu mwenezi msitaafu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Humphrey Polepole amehoji ni kwa nini watanzania wanataka kuacha mbinu za asili zilizotusaidia mwaka jana kupambana na corona na tukaibuka na mafanikio makubwa kiuchumi na kijamii?

Bwana Polepole ametolea mfano wa nchi zote zilizojaribu kupambana na Corona kwa kufuata mfumo wa kimagharibi mwishoni wa mwaka 2020 ziliishia kupata ukuaji hasi wa uchumi kwenye nchi zao!

Polepole amesema ni Tanzania tu ndiyo iliyopata ukuaji wa uchumi chanya kwenye nchi zote za Afrika mashariki. Sasa kwa nini sisi watanzania tunaona aibu kujivunia hizo mbinu za asili? Amehoji mh Polepole.

Mwaka jana tulipambana na Corona kwa kutumia njia tatu.
1. Kumtanguliza Mungu mbele
2. Kufuata mbinu mbalimbali tunazoshauliwa na watalaamu wetu
3.Kuchapa kazi kwa bidii

Jiwe Bupiji na Nyungu havikumsaidia na Covid-19 ikamtuliza.
Mamaake Slow Slow Covid-19 imemshughulikia.
Huyo Chakubanga anasikilizwa kwa sasa na MATAGA wenye Mtindio wa Ubongo
 
Na waliotumia njia za kisasa na bado wamekufa kuliko sisi nao tusemeje?
Covid-19 so Far imeua Raisi Mmoja aliyeko Madarakani
Raisi huyo Ali underplay Covid-19 ,.ikamlaza Kaburini
 
Wale madalali wa chanjo hawawezi kuelewa hii. Watafura kama vifutu.

Chanjo ya beberu iko njiani, na wao walishapokea mapesa ya udalali.

Ukiwaeleza habari za mimea-tiba ama tiba-asili wanafyumu na kusonya kwa ghadhabu.

Madalali wa corona hawa. Hawatusumbui.
Mimea Tiba haikumsaidia Jiwe ?
 
Pole kwakufiwa lakini ebu sema huko kwingine hawakufa? Mbona sisi hali yetu ni afadhli kuliko wao?
Kwenu Afadhali kwani mnatoa Stats / Data ?
Fala kabisa
 
Waliokufa Kwa Corona waliotumia hizi mbinu za Kienyeji tunasemaje. Dada yangu alijufukiza, akala Nimcaf yet she died from Corona. RIP my sister. Hapa Tanzania tuseme tuu kuna Nguvu ya Mungu tusioielewa.
Mkuu, hata huko walikotumia mbinu za kimagharibi bado kuna watu walikufa, tena wengi zaidi! Pole kwa kufiwa na dada.
Mbinu zetu zimetusaidia sana.
 
Waliokufa Kwa Corona waliotumia hizi mbinu za Kienyeji tunasemaje. Dada yangu alijufukiza, akala Nimcaf yet she died from Corona. RIP my sister. Hapa Tanzania tuseme tuu kuna Nguvu ya Mungu tusioielewa.
Nguvu ya Mungu tusiyoielewa... I agree with you!
 
1623886850715.png
 
Waliokufa Kwa Corona waliotumia hizi mbinu za Kienyeji tunasemaje. Dada yangu alijufukiza, akala Nimcaf yet she died from Corona. RIP my sister. Hapa Tanzania tuseme tuu kuna Nguvu ya Mungu tusioielewa.
Mungu akili zake hazichunguziki, kumtanguliza Mungu mbele ndio mpango mzima.
 
Back
Top Bottom