Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Waziri Mkuu wakati huo Mizengo Pibda aliwahi kusema hivyo hivyo na bado Zitto akapera uchaguzi uliofuata. Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Kama ni kwa nguvu ya wananchi sawa, ila kama ni kwa nguvu ya dcm, napata mashaka kidogo
 
Kuna muingiliano wa madaraka, na baadhi ya viongozi wa chama kujisahau na kudhani wanaongoza serikali. Polepole hastahili kabisa kukagua na kuagiza watekelezaji wa miradi ya serikali. Lakini kwa kuwa ni siasa za kuzomeana, tunawasikia wakijiaminisha serikali ni yao. Serikali ikishaundwa siyo mali ya chama.

Hata hivyo jambo moja la kushangaza ni jinsi Polepole alivyojionyesha kutoka mtu aliyedhaniwa kuwa na uwezo wa fikra hadi mtu asiyeweza kabisa kupambanua mambo. Alivyo sasa hivi ni kama ana bahatisha mambo. Au, tatizo ni vyombo vya habari vilivyomuonesha kama kijana anayeweza kumbe anakumbuka tu yale aliyo kariri shuleni. Anakatisha tamaa!!!!!
 
Mpaka 2020 kwani project yake ya kununua madiwani na wabunge imephase out?
Hii zana ya kununua ni kichaka kipya cha ufipa boys kujificha ili wapate nafuu wakati chama kinateketea.

Stop this nonsense .
 
Hii ni kweli kabisa. Nitafanya kazi ya Urais
Bw. Zitto anayoyasema Polepole, anamaanisha. Kiasi hata wewe ulikuwa mgumu wa kuenda na wakati, na ukajitenga na wenzako. Tangu Rais huyu anaaanza, wenzako walisusia hotuba yake kwa Bunge, wewe ukatofautiana na wenzako. Ukishakuwa pamoja na adui, ujue aliyeko pembeni hakutofautishi na adui yako. Itakuwa vigumu sana wana Kigoma kukutofautisha na CCM.
 
Si hairuhusiwi Kufanya Siasa?
Huyu Mbona anazunguka daah hata sielew kwakweli..
 
Watu wa Kigoma hawadanganyiki kirahisi,Ngoja tusubiri hiyo 2020 tukiwa hai tutashuhudia
 
Polepole anaamini kwamba siasa ndio ajira pekee !
 
Si hairuhusiwi Kufanya Siasa?
Huyu Mbona anazunguka daah hata sielew kwakweli..
Kwa kuwa yeye ni chama tawala kilichopewa dhamana na watanzania na anawajibu wa kuihoji na kuisimamia Serikali vilivyo...!Sasa zitto anamuiga kwa kutaka kwenda kukagua miradi isiyomhusu huku akikwepa kutokea kwenye vikao vya baraza la madiwani kwenye halmashauri yake.
 
Zito ajikite kunako kilimo cha umwagiliaji maana cha kutegemea mvua na kama kufanya siasa tu.
 
Tulia usome kwa umakini uelewe si kukimbilia kujibu
 
Wapiga kura wamemkataa?. Afunguke zaidi maana kilichomo kwenye box hatukijui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…