Uchaguzi 2020 Polepole: Zitto Kabwe atafute kazi nyingine, 2020 hatarudi Bungeni

Huyu bwana slowslow anamuogopa sana mkulu ndo mana anafanya ujinga anaopenda mkulu.
 
Hivi anachofanya polepole sio siasa? Maana siasa zimezuiwa hadi 2020!!!
 
Kuendelea kuona kuwa wapinzani ni maadui wa nchi hii hamtafanikiwa kamwe kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli
Hivi una anzia wapi kuwaamin baadhi kuwa siyo maadui wanapofikia kuitaka jumuiya ya kimataifa ituwekee vikwazo vya kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kadhalika....unaanzia wapi kuwaamini baadhi wanapoamua kwenda nchi ya jirani na kutumia vyombo vya nchi hiyo kuisema vibaya serikali ya nchini mwao...unaaazia wapi, na kuuliza.
===
Upinzani kuna baadhi ya watu muhimu sana wanaoitakia mema nchi yetu lakini wanazimwa na hawa ambao wanatupa mashaka ya uaminifu wao kwa nchi kwa maneno yao na matendo yao na wana sauti kweli hawa.
 
Sio Zitto tuu

Tunajua agenda yenu ccm ya kutumia vyombo vya usalama ili kuua upinzani wote

Ndio maana tunataka kukomesha huu upumbavu ifikapo 26/4/2018
 
kwani slow slow ana kura ngapi atakazopiga huko kigoma?
 
POLEPOLE usijidanganye ccm inachukiwa na ndio Maana anatumia nguvu kushinda
 
2020 polepole ajiandae atuachie chama chetu tumemchoka ebo
 
Zitto atakoma kuwa mbunge ikiwa tu wale wazee wa pale Kigoma watakapo sema hawamhitaji kwa sasa,lakini sio kwa kauri ya Pole pole
 
Kasi ya rais magufuli itafagia upinzani uchwara wengi 2020.
Kasi gani? Kuchukua pesa za Umma, pesa za walipa kodi kuwanunua Wapinzani, kurudia chaguzi? Pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo ni kubwa sana ni pesa ambazo zingeweza kujenga Hosptal za rufaa kila mkoa na kuajiri madaktari toka India na wagonjwa wote wakatibiwa nchini pasipo kupelekwa nje,
 
Mabilioni anayovuna kwenye huu mradi haramu wa kununua wapinzani uchwara yamempa kiburi sana huyu chakubanga.
Mladi wa ununuzi wapinzani, kurudia uchaguzi, Uchakachuaji,wizi wa kura, kuwabambikia kesi, kuwapiga Risasi akina Lisu, kuwafunga jela akina Sugu ni mladi haramu wa pesa za walipa kodi lakini Madalali wa siasa huko CCM wameneemeka mpaka wamejitoa fahamu kwa kiwango cha kutisha
 
Kweli kasi ya kuteka na kupiga watu risasi, kununua wapinzani ni aibu kwa ccm
Kibaya wanakula pesa za Umma, pesa za walipa kodi ambao ni watanzania wote, Wageni toka nje na watu wasio na vyama, pesa zao zinachukuliwa Hazina kienyeji na kutumika kwa mambo ya hovyo hovyo tu, ni Ufisadi na ufujaji wa pesa za Umma kwa kazi haramu za kienyeji zisizo na tija wala kujulikana.
 
PolePole hajakosea kwa sababu ubunge wa Zitto wa 2015 ulifanikishwa na CCM. Bila maagizo ya ccm Zitto alikuwa ameshaanguka ubunge Kigoma mjini. Akamuulize Kafulila kwa sababu hayo ndio yafuatayo Kigoma Mjini 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…