Polisi: Idris Sultan anashikiliwa kwa kujaribu kuharibu ushahidi na makosa mengine ya kimtandao

Polisi: Idris Sultan anashikiliwa kwa kujaribu kuharibu ushahidi na makosa mengine ya kimtandao

Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumshikilia Idris Sultan aliyekamatwa Jumanne iliyopita akihusishwa na tuhuma za makosa ya kimtandao likiwemo la kujaribu kuharibu ushahidi.

Mchekeshaji huyo alikamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar ambako alihojiwa kwa kutuhuma za uonevu wa Kimtandao ikiwa ni siku chache baada ya kuweka picha ya zamani ya Rais Magufuli iliyoambatana na video yake akicheka.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Tunaendelea kumshikilia kwasababu kubwa mbili; moja ni kuwa baada ya kutakiwa kuripoti Polisi alijaribu kuharibu ushahidi na pili ni katika upelelezi wetu tumebaini makosa mengine ya Kimtandao aliyokuwa akiyafanya”

Pia, ameongeza “Katika mahojiano tuliyofanya naye tulibaini alitumia namba ya simu isiyo yake katika kutenda uhalifu huo hivyo ushirikiano wake ndio utakaomfanya aendelee kukaa kituoni.

Lakini pia Wakili wake, Benedict Ishabakaki amesema baada ya mteja wake kuhojiwa walielezwa kuwa dhamana ipo wazi lakini kila wakifuatiliwa wanazungushwa.
Nachelea kusema kwamba hata wakili wake kazubaa kwa kiasi flani. Yapo maombi maalumu yaitwayo "habeas corpus" kwa lugha ya Kilatini, au "bring the body before the court" kwa Kingereza.

Haya ni maombi maalum ya kulilazimisha jeshi la Polisi limpeleke mtuhumiwa Mahakamani ili Mahakama ione kama anastahili kunyimwa dhamana au anaonewa, tena akitaka raha anaweka na "certificate of urgency" au "hati ya dharura" ili maombi hayo yasikilizwe kwa uharaka, sasa wakili wake anasubiri nini?!
 
Nachelea kusema kwamba hata wakili wake kazubaa kwa kiasi flani. Yapo maombi maalumu yaitwayo "habeas corpus" kwa lugha ya Kilatini, au "bring the body before the court" kwa Kingereza.

Haya ni maombi maalum ya kulilazimisha jeshi la Polisi limpeleke mtuhumiwa Mahakamani ili Mahakama ione kama anastahili kunyimwa dhamana au anaonewa, tena akitaka raha anaweka na "certificate of urgency" au "hati ya dharura" ili maombi hayo yasikilizwe kwa uharaka, sasa wakili wake anasubiri nini?!
Mawakili wanaoshinda Tweeter na Instagram hao maneno meengi.
 
Kijana ndoto zake zinapotezwa hivi hivi. Haki itendeke huenda yote aliyotuhumiwa kusiwe na kosa

Sent using Jamii Forums mobile app

Idris ameshindwa kutofautisha vitu vya kufanyia utani na vitu gani si vya kufanyia utani kama huo aliokuwa akiufanya. Mwanzo napo alifanya kosa kama hilo lakini bado hakujifunza.
Mie naomba akae humo hata mwezi alfu wamwache labda akili itamkaa vizuri.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nchi ina tamaduni zake ukienda Saudi Arabia kunywa pombe hadharani ni kutafuta ugomvi na mamlaka (hata kama kwenye jamii zingine ni jambo la kawaida) na kila mtu duniani anaelewa ukijitia mkaidi ukafanya tofauti yatakayo kukuta wa kujilaumu ni wewe mwenyewe.

Ukienda nchi zenye blasphemy laws unatakiwa kujua mipaka yako.

Similarly waafrika pia tuna culture zetu hatuna utani, tamaduni za kujibizana na wazee wetu na mambo mengine ya heshima.

Ingelikuwa kipanya kashikwa kwa ku ridicule maamuzi ya serikari aliyofanya kiongozi kupita utaratibu wake hapo kuna hoja ya freedom of speech.

Lakini mtu anaibuka na kutaka kuleta utani na mtu anaeweza kumzaa inawezekana ni sawa kwa wengine lakini si utamaduni wa kiafrika (sio tanzania tu) binafsi mpaka sasa sina utani utakaomkera kaka yangu mkubwa wala dada zangu walionizidi let alone wazazi wangu wangekuwa hai.

Mi sioni hoja za watu wanaomtetea huyu mtoto serikali ina kila sababu ya kulinda tamaduni zetu, wacha wamtie adabu vijana wengine wasijaribu atuwezi kuiga culture za wenzetu kwenye kila kitu.
 
Akitoka lupango ukimuonyesha picha ya Magu lazima atoke nduki[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom