tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Hivi sasa tuna majimbo? Kila sehemu sheria zao.Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limepiga marufuku, magari yanayosafirisha abiria kufanya safari usiku wa zaidi ya saa sita na kwamba atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema: “Ukiwa unatokea Dar kama hesabu zako zitakuonesha kuwa utafika Mkata zaidi ya saa sita usiku, ujue mtaalala hapo hamtapita.
“Hatua hiyo ni kutokana na wimbi la ajali katika barabara ya Tanga - Segera, hii itahusu magari yote ya abiria.”
Chanzo: Millard Ayo