tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Hivi sasa tuna majimbo? Kila sehemu sheria zao.Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limepiga marufuku, magari yanayosafirisha abiria kufanya safari usiku wa zaidi ya saa sita na kwamba atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema: “Ukiwa unatokea Dar kama hesabu zako zitakuonesha kuwa utafika Mkata zaidi ya saa sita usiku, ujue mtaalala hapo hamtapita.
“Hatua hiyo ni kutokana na wimbi la ajali katika barabara ya Tanga - Segera, hii itahusu magari yote ya abiria.”
Chanzo: Millard Ayo
Acheni uendeshaji wa hovyo wa vyombo vya motoNchi ngumu sana hii.
Tutafanya hivyo mkijifunza kuzingatia sheria za usalama barabarani.Mwisho wa siku suala la Magari ya abiria linapaswa kuwa centralized. Na wayaruhusu kufanya safari 24hrs.
Hao polisi wanawaambia majambazi kwamba kuanzia saa 6 wao hawapo kwa hiyo ni zamu ya majambazi.Mimi nishazoea nafanya mishe zangu mpaka saa mbili usiku nasogea hapo Kibo ubungo, nakamata kosta mpka njia panda.
Sasa haya Matamko vipi tena
... katazo linayahusu magari ya misiba?
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limepiga marufuku, magari yanayosafirisha abiria kufanya safari usiku wa zaidi ya saa sita na kwamba atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema: “Ukiwa unatokea Dar kama hesabu zako zitakuonesha kuwa utafika Mkata zaidi ya saa sita usiku, ujue mtaalala hapo hamtapita.
“Hatua hiyo ni kutokana na wimbi la ajali katika barabara ya Tanga - Segera, hii itahusu magari yote ya abiria.”
Ajali zenyewe zinatokea mchana kweupee
... hili linatakiwa kuwekwa clear maana magari mengi ya misiba (coasters, etc.) yanakuwa yamebeba abiria (unless by definition hao sio abiria). Kuulaza msiba barabarani tangu saa 6 hadi 12 ndipo safari ianze ina changamoto zake.Hapana
... hili linatakiwa kuwekwa clear maana magari mengi ya misiba (coasters, etc.) yanakuwa yamebeba abiria (unless by definition hao sio abiria). Kuulaza msiba barabarani tangu saa 6 hadi 12 ndipo safari ianze ina changamoto zake.
ugumu wa nchi kawaida sema watu ndo vichwa vigumu Kama mtoa OdaNchi ngumu sana hii.
Jee, ni halali kila mji kujiwekea sheria zake? Miaka ya 80 sheria ilipitishwa kukataza usafiri wa usiku kwa nchi nzima. Hilo sawa kwa kuwa lilihusu nchi nzima. Hili la kuweka sheria zinazohusu mji mmoja mmoja lina utata. Kwa mfano gari la abiria linatoka Mbeya kwenda Tanga likaharibika kilomita 100 kutoka Tanga; wakalishughulikia likatengamaa saa sita kasoro za usiku. Ni halali hilo gari kuendelea na safari kutoka hapo lilipoharibikia mpaka ukingoni mwa Tanga halafu hapo lisiendelee kwa kuwa saa sita usiku itakuwa imegonga tayari?