Polisi sasa wanawakamata wanaume wanaowanunua dada poa, wanawake hawakamatwi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa sehemu ya mikakati yake katika kuzuia biashara ya wanawake kujiuza ni kuwakamata wanaume ambao wanahusika katika biashara hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ameamua kuja na staili tofauti ambayo haitahusisha matumizi ya nguvu kwa wanawake wanaofanya biashara hiyo.

“Kuna sehemu tuliweka kambi kwa siku tatu, hatukuwakamata wanawake amao walikaa pale wakipigwa na baridi kwa siku zote hizo, wanaume hawakutokea na ndiyo tuliokuwa tukiwasubiri, baada ya kuona hakuna wateja wanawake hao hawakurudi eneo hilo.

“Nimeelekeza na kuagiza wanaume wakamatwe kwa kuwa kama hawataenda maeneo hayo basi hiyo biashara haitakuwepo,” - Muliro.

Chanzo: Wasafi FM
 
Hivi kamanda kamaliza mtandao wanaouza madawa ya kulevya? Wizi wa simu, TV vifaa vya magari, pikipiki, wizi wa kwenye mtandao, utapeli?
Leo unakwenda kudeal na watu wazima kwa hiari yao wenyewe wanakubalina kufanya mapenzi kwa malipo.
Ukweli mwanaume nalipia mapenzi direct or indirect.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa sehemu ya mikakati yake katika kuzuia biashara ya wanawake kujiuza ni kuwakamata wanaume ambao wanahusika katika biashara hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ameamua kuja na staili tofauti ambayo haitahusisha matumizi ya nguvu kwa wanawake wanaofanya biashara hiyo.

“Kuna sehemu tuliweka kambi kwa siku tatu, hatukuwakamata wanawake amao walikaa pale wakipigwa na baridi kwa siku zote hizo, wanaume hawakutokea na ndiyo tuliokuwa tukiwasubiri, baada ya kuona hakuna wateja wanawake hao hawakurudi eneo hilo.

“Nimeelekeza na kuagiza wanaume wakamatwe kwa kuwa kama hawataenda maeneo hayo basi hiyo biashara haitakuwepo,” - Muliro.

Chanzo: Wasafi FM
Iko wapi haki ya mwanaume mbona kila kukicha nchi inamkandamiza mwanaume , oo Tuamke wanaume vita imetufika sasa
 
Kamanda wangu Muliro namuheshimu sana maana pia ni Mwalimu wangu nilipokuwa Depo CCP 1998,yeye kipindi hiko alikuwa Inspekta pale akiwa Mkufunzi,naamini kazi hiyo ya ku-deal na Dada poa HATAKUJA kuiweza,ni vema awekeze nguvu kubwa kwenye kupambana na Uhalifu mwingine na sio hao Dada poa
Sema wa Depo!
 
Wazuie kwanza wizi WA vifaa kwenye Magari, simu, utapeli, Mitandao, majambazi ndio waanze na hayo ya ziada ambapo mtu Kwa hiari yake anaamua kuudhalilisha mwili wake!! Hii biashara ipo Dunia nzima aache kiwapotezea polisi muda!! Maofisa ustawi WA jamii watoe elimu ya madhara, je anamkubuka ahabu!? Hata mamlaka zilikuwa hazimsimbui!! Pia hii ni tiba Kwa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji watoto
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa sehemu ya mikakati yake katika kuzuia biashara ya wanawake kujiuza ni kuwakamata wanaume ambao wanahusika katika biashara hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ameamua kuja na staili tofauti ambayo haitahusisha matumizi ya nguvu kwa wanawake wanaofanya biashara hiyo.

“Kuna sehemu tuliweka kambi kwa siku tatu, hatukuwakamata wanawake amao walikaa pale wakipigwa na baridi kwa siku zote hizo, wanaume hawakutokea na ndiyo tuliokuwa tukiwasubiri, baada ya kuona hakuna wateja wanawake hao hawakurudi eneo hilo.

“Nimeelekeza na kuagiza wanaume wakamatwe kwa kuwa kama hawataenda maeneo hayo basi hiyo biashara haitakuwepo,” - Muliro.

Chanzo: Wasafi FM
👏Ukitaka kutibu ugonjwa jua chanzo cha ugonjwa halafu shambulia hicho chanzo utakuwa umezuia ugonjwa huo ( preventive measures)

👏Kwa hili wanachokifanya mapolisi nawapa kongole kubwa kwa sababu ukizuia wanunuzi wauzaji hawatakuwepo ( Demand supply theorem)
 
Tandika kwa wahaya pale Polisi hawajafika?

Pale ni aibu ya taifa hasa mwezi huu wa Ramadhani na mfungo wa Kwaresma wapelekwe polisi wa kutosha ikiwezekana defender kabisa Kumi maana ni wengi na tule tuvijumba twao kule wangedaka wanaume kibao
 
Back
Top Bottom