Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

Wakristo ijumaa kuu tunaadhimisha kifo cha Bwana Yesu, na alfajiri ya jumapili tunasherekea kufufuka kwake, sasa inakuwaje tunalazimishwa kutii sheria za wanadamu halafu tuzidharau za MUNGU?. Tunaomba sana jeshi lifikirie tena kabla ya kutoa hizi amri zao,msipuuze imani za watu wengine kisa mna imani zenu,Hatusherekei kwa kuwa ni uamuzi wetu tu bali ni maa maandiko yanasema shangilieni BWANA amefufuka.
Na kabla hajafa Mh Magufuli..ibada na sherehe zilikuwapo. Vipi kifo chake kipelekee kututoa kwenyebimani zetu?
 
Jeshi la polisi nchini limewataka waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku wakikumbuka bado Taifa liko katika siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amesema, Jeshi hilo halitarajii kuona sherehe na shamrashamra kama ilivyozoeleka kila inapofika sikukuu hiyo, lengo likiwa ni kuendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga vizuri kuhakikisha Waumini wa dini ya Kikristo wanashiriki ibada ya Ijumaa Kuu, ibada ya mkesha wa Pasaka siku ya Jumamosi na Ibada ya Pasaka siku ya Jumapili katika mazingira ya amani, utulivu na usalama na Wananchi wengine wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Ameziomba kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini katika suala zima la kudumisha amani, ulinzi na usalama.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime, pia amewahakikishia Watanzania wote kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari, ingawa kuna matukio machache ya kiuhalifu wa kijinai na ajali za barabarani, mambo yanayoendelea kushughulikiwa.
Hili agizo unakitoa wapi?? Kama ni Kwa Raisi wetu sawa ila kama ni kwa mkuu wa polisi..mwambie hajatutendea haki. Hapo anatutafuta ubaya.
 
Nimeiona clip ya msemaji wa jeshi la polisi mtandaoni akitangaza kuzuiwa kwa wakristo kutokushangilia ushindi wa Masihi yaani Yesu Kristo kukishinda kifo na kufufuka kutoka wafu. Pasaka Ina maana kubwa Sana kwa wakristo kwani Imani yao kwa Mungu inaanzia hapa.
Ombi langu kwa serikali itoke hadharani na kukanusha angazo hili la kuzuia sherehe za pasaka kwa sababu ya taifa kuwa kwenye maombolezo kwani havihusiani!
Povu linakaribishwa kwani Nina nguo chafu zinahitaji sabuni na itapendeza likiwa la omo!
 
Wamezuia kwenda kanisani, kuchinja kuku au kucheza wimbo wa Baba lao? Tujuzane
 
Jeshi la polisi nchini limewataka waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Pasaka huku wakikumbuka bado Taifa liko katika siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amesema, Jeshi hilo halitarajii kuona sherehe na shamrashamra kama ilivyozoeleka kila inapofika sikukuu hiyo, lengo likiwa ni kuendelea kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.

Amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga vizuri kuhakikisha Waumini wa dini ya Kikristo wanashiriki ibada ya Ijumaa Kuu, ibada ya mkesha wa Pasaka siku ya Jumamosi na Ibada ya Pasaka siku ya Jumapili katika mazingira ya amani, utulivu na usalama na Wananchi wengine wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Ameziomba kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini katika suala zima la kudumisha amani, ulinzi na usalama.

Msemaji huyo wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime, pia amewahakikishia Watanzania wote kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari, ingawa kuna matukio machache ya kiuhalifu wa kijinai na ajali za barabarani, mambo yanayoendelea kushughulikiwa.
Polisi,
Wakristo hawasherehekei kifo (Mauti) wanasherehekea kufufuka (Ufufuo) wa Kristo. Kwa maana hiyo Ijumaa wanahuzunika kwa kifo cha mwokozi wao na jumapili wanasherehekea ushindi wa mwokozi wao dhidi ya mauti. Mnapowakataza kufurahia ushindi wa Kristo mnamtukuza shetani.
 
Nimeiona clip ya msemaji wa jeshi la polisi mtandaoni akitangaza kuzuiwa kwa wakristo kutokushangilia ushindi wa Masihi yaani Yesu Kristo kukishinda kifo na kufufuka kutoka wafu. Pasaka Ina maana kubwa Sana kwa wakristo kwani Imani yao kwa Mungu inaanzia hapa.
Ombi langu kwa serikali itoke hadharani na kukanusha angazo hili la kuzuia sherehe za pasaka kwa sababu ya taifa kuwa kwenye maombolezo kwani havihusiani!
Povu linakaribishwa kwani Nina chafu zinahitaji sabuni na itapendeza likiwa la omo!
Waache maPoliCCM wamzike mfu wao ambaye hatafufuka milele sisi Wakristo tuendelee na sherehe za ufufuo wa Bwana Wetu Yesu Kristo aliye hai.
 
Si hua mnasema vyuma vimekaza na Sikukuu za siku hizi ni kama siku za kawaida tuu?

Imekuaje tena ghafla tuu?

Nauliza tu.
 
Tanzania ina viongozi wajinga sana!Huwezi kuingilia masuala ya imani za watu!!They are very stupidy!Ina maana Magufuli ni mkubwa na ni mkuu kuliko Yesu ambae anatarajia kufufuka siku ya Pasaka?!
 
Habari ndio hiyo mliojipanga kusheherekea tafuteni shughuli za kufanya.
20210401_210217.jpg
 
Polisi,
Wakristo hawasherehekei kifo (Mauti) wanasherehekea kufufuka (Ufufuo) wa Kristo. Kwa maana hiyo Ijumaa wanahuzunika kwa kifo cha mwokozi wao na jumapili wanasherehekea ushindi wa mwokozi wao dhidi ya mauti. Mnapowakataza kufurahia ushindi wa Kristo mnamtukuza shetani.
Mwanakondoo ameshinda🙏 hallelujah
 
Back
Top Bottom