Polisi: Tumewakamata watuhumiwa waliokula njama ya kutaka kumteka Tarimo - Kiluvya

Polisi: Tumewakamata watuhumiwa waliokula njama ya kutaka kumteka Tarimo - Kiluvya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
PRESS KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA UTEKAJI_page-0001.jpg

PRESS KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA UTEKAJI_page-0002.jpg



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na operasheni maalum kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Kwa ujumla hali ya usalama Dar es Salaam inaendelea vizuri.

Pia soma: Watuhumiwa waliotaka kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) wafikishwa Mahakamani

Tarehe 11 Novemba, 2024 eneo la Kiluvya Ubungo Dar es Salaam lilitokea tukio la kutekwa kwa Bw. Deogratius Tarimo, mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani. Kufuatia tukio hilo na mengine ya nyuma Polisi Dar es salaam imekuwa ikiendelea kuchunguza na kufuatilia taarifa mbalimbali pia kukusanya ushahidi wa kisheria kuhusiana na matukio hayo ili kuyazuia.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imefanikiwa kukamata kundi la wahalifu wanane wanaotuhumiwa kula njama kwa pamoja na baadae kufanya tukio la kumteka Deogratius Tarimo. Wat uhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti Dar es salaam, Songea Ruvuma na eneo la Mbingu Mlimba Morogoro. Pia lilipatikana gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa tukio hilo huku ikitumia namba isiyo halisi T 237 EGE na baada ufuatiliaji namba halisi ya gari hiyo ni T237 ECF.

Watuhumiwa hao ni :-

1. Bato Bahati Tweve, Bondia, Miaka 32, Mkazi wa Kimara Bunyokwa na Songwe Mbozi

II. Yusuph Abdallah, Miaka 32, Mkazi wa Mbingu - Mlimba Morogoro

III. Fredrick Juma, Miaka 31, Mkazi wa Kibamba

IV. Nelson Elimusa msela, Dereva Tax, Miaka 24, Mkazi wa Mbezi Luguluni

V. Benk Daniel Mwakalebela@tall, Miaka 40, Mkazi wa Mbezi Makabe na Kyela Ipinda

Rusungo Mbeya

VI. Thomas Ephraim Mwakagile @ baba mage Bunyokwa na Kyela Ngonga Ndiali Mbeya Miaka 45, Mkazi wa Kinyerezi

VII. Anitha Alfred Temba, Miaka 27, Mkazi wa Mbezi Mwisho.

VIII. Isack Mwaifani, @ boxer, Mkazi wa Kimara Tembo Salanga na Bujonde Isanga Kyela Mbeya

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi ya kuzuia vitendo vya kihalifu lakini pia kuwakamata na kutokuwa na huruma kwa watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio ya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria kwa kuwapeleka kwenye mamlaka zingine za haki.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za kweli ili Jeshi lichukuwe hatua za kisheria kwa watu wanaopanga kufanya matukio ya kihalifu ili washughulikiwe mapema kabla ya matukio.

Imetolewa na;
Muliro J. Muliro -SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam
www.polisi.go.tz
www.twitter.com/tanpol
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na operasheni maalum kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Kwa ujumla hali ya usalama Dar es Salaam inaendelea vizuri...
Picha zao please Ili wale waliokuwa wanaeneza picha za uongo Twitter washughulikiwe nao.
 
Safi,na hongera kwa jeshi la police..naona cheni imeongezeka apo hadi kufika watu 8 tofauti nawale wachache tuliowaona kwene video crip,hii inaonyesha bwana Tarimo alitoa maelezo yaliyounganisha dot yakumpata mhusika mkuu aliyewatuma vijana
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linaendelea na operasheni maalum kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Kwa ujumla hali ya usalama Dar es Salaam inaendelea vizuri...
Wanyakyusa huwa wanapenda sana kujihusisha na uhalifu halafu ni vijana wa kyela.hao wabanwe ovaries ili wataje nani anayewatuma na kwa maslahi ya nani pia.
 
Kwenye video walikuwa wangapi ? Naona kama idadi imezidi🐼
Waliopanga njama wanaweza kuwa hata 100 wakagawana majukumu, wengine kufatilia ratiba, wengine kuteka, wengine kutoa kipigo. Kwahiyo hao wa kwenye video walipewa majukumu ya kuteka. Wengine walikuwa na kazi zingine ndo maana hukuwaona kwenye video
 
Back
Top Bottom