Polisi hawana mamlaka ya kuhukumu nani ni muhalifu, polisi wanatuhumu tu, mahakama ndiyo inayohukumu.
Kauli hii ya Polisi imefanya makosa ya kutoa hukumu.
Tumeona mifano sehemu nyingi, mfano Amadou Diallo, muhamiaji aliyepigwa risasi na polisi New York City. Amadou Diallo alipigwa risasi akitoa wallet yake mfukoni, pilisi wakafikiri anataka kuwapiga risasi.
Sasa huko Tanzania ambako hakuna uwazi na ufuatikiaji, tutajua vipi wanachosema polisi ndiyo kweli na si cover up?
Ukiunga mkono Polisi kufanya hizi summary execution, jiulize kama tukiruhusu polisi kuua watu hivi, haitawezekana kwa raia wasio na hatia, hata wewe, kuuawa na polisi kwa kubambikiwa tu u panya road na watu wasiokupenda?