Polisi: Vijana wawili waliouawa Vingunguti, Dar ni Panyaroad

Polisi: Vijana wawili waliouawa Vingunguti, Dar ni Panyaroad

Kutokana na Mazingira ya tukio lenyewe pamoja na shuhuda ambazo tayari zimetolewa hadi leo hii kuhusiana na tukio hili, haikufaa tena kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa kama hii waliyotoa, ambayo inakinzana na matakwa ya Sheria za nchi hususani suala zima la Utawala Bora wa Sheria. Polisi walipaswa kukaa kimya bila kusema kitu kingine chochote kile zaidi ya shuhuda ambazo tayari zimetolewa na Wananchi wahanga.
Kuna mwingine panyaroad kakimbia anaitwa panya white ndio wewe Nini?
 
Polisi wanaofanya kazi nzuri kuzuia vibaka, Kinga ni Bora kuliko tiba
 
Kutokana na Mazingira ya tukio lenyewe pamoja na shuhuda ambazo tayari zimetolewa hadi leo hii kuhusiana na tukio hili, haikufaa tena kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa kama hii waliyotoa, ambayo inakinzana na matakwa ya Sheria za nchi hususani suala zima la Utawala Bora wa Sheria. Polisi walipaswa kukaa kimya bila kusema kitu kingine chochote kile zaidi ya shuhuda ambazo tayari zimetolewa na Wananchi wahanga.
Hii kitu hakuna msalie mtume Wala mpiga kengere kanisani.Hakuna haki Wala utawala wa Sheria Kwa panyarodi,hii watu ni wakatili sana na bora muda mwingine tuwapongeze na kuwatia moyo polisi wetu Kwa kazi iliotukuka.Nenda Saudi Arabia ukajionee ukubwa wa uharifu umepungua sana wastani wa matukio zero hii ni kutokana na kula chuma,kisu Cha shingo au kunyongwa.
 
Kwa taarifa hii ya Polisi, Je, wanatoa ujumbe gani kwa umma hususani kuhusiana na suala la utawala bora wa Sheria na Utii wa Sheria bila shuruti????
Kwa maoni yangu na kwa kuzingatia hali halisi iliyopo kuhusiana na tukio hili, naona yafaa Jeshi la Polisi lingekaa kimya kuhusu tukio hili. Lisingetoa taarifa kama hii ambayo ukiitathmini kwa kina ina walakini na ukakasi mwingi, naona kama inahamasisha Wananchi ili wajichukulie Sheria mikononi.
Wamefanya kitu sahihi.

Hao raia wenyewe nasikia walikuwa washachoka, watu wameuliwa wengine walemavu.

Ni sawa kabisa, watu wanawaza kupambana maisha wapumbavu wachache hawwtaki kufanya kazi wanaendekeza usela wa kijinga.
 
Wamama kama nyie ndo maharibu watoto, mtoto mwizi bado unamlea Lea fanya mpango ww kumpa hata fimbo au mpeleke polisi akachapwe viboko
Tena hata akisikia kwamba mwanae ni mwizi hataki kumuonya na toto ndio linazidi kuharibikiwa.
 
Nyie mnaongea tu,mi nilipigwa roba ya mbao migo pale morocco hotel.
Wakalamba jumla mil+.
Bahati mbaya au nzuri kuna saa nilipewa zawadi nayo waliiba.
Sasa siku 2 nyingi naletewa saa ileile inauzwa kwangu.
Saa yangu mwenyewe breitling.
Nikasema ngoja nilete hela.
Kumbe najitwika silaha zote.
Ikawaa kaa chini.
Nani kakupa saa?
Piga bapa 3 katafuta njia mwenyewe.
Nikamwambia kaa chini hapo na utulie.
Pigia masela wangu kino wakaja kama 10 hivi.
Tulienda kuwatengeneza wale jamaa mpk mama zao walikua wanakuja kuomba poo.
Hela haikurudi ila tulibeba kila kitu chenye value na vidonda juu.
Sa ingine civil justice inabidi ihusike.
 
Kama kweli ni panya road nawapongeza jeshi la polisi na kuhimiza wananchi wenzangu kuendelea kujichukulia sheria mkononi kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote ile.
Naunga mkono hoja.

Wapumbavu wachache wameamua kuharibu maisha yao Kwanini wasife watupishe.

Day waka za bodaboda zipo kibao hawataki kufanya kazi, waende hata kwa mo au bakhresa wafanye vbarua hawataki hawawezi.

RAIA IKIWEZEKANA WAUE, POLISI WAMEFANYA KAZI NZURI KAMA NI PANYA ROAD.
 
Bado nina hasira na hawa watu,jamaa wawili walikuwa na boda juzi nilikuwa nafanya mazoezi wakanichapa mgongoni na kitu nahisi ni waya au ubao,wakakimbia sijui lengo lao lilikuwa ni nini...
 
Bado nina hasira na hawa watu,jamaa wawili walikuwa na boda juzi nilikuwa nafanya mazoezi wakanichapa mgongoni na kitu nahisi ni waya au ubao,wakakimbia sijui lengo lao lilikuwa ni nini...
Ungewapigia yowe la mwizi [emoji1787]
 
Mage dada yangu kama kweli polisi waligundua ni waovu naona pia wameuawa kistaarabu sana, nafikiri hujawahi kuona unyama wa hali ya juu wanaofanya hawa vibaka sio?

Basi yeyote ambaye aliwahi kukutwa na dhahama ya vibaka atakushangaa sana sana ,jamaa yangu mpaka leo haongei vizuri walitaka kumchinja bahati nzuri watu wakatokea wakiwa washaanza ,hao sio wa kwenda kulimishwa hawastahili kuishi.
NAUNGA MKONO HOJA!

Kama ni panya road ni sawa kabisa, kuna mshkaji hana mikono yote ilikatwa alikuwa anarudi kutoka zake mihangaiko.

Wafe tu.
 
Kwa taarifa hii ya Polisi, Je, wanatoa ujumbe gani kwa umma hususani kuhusiana na suala la utawala bora wa Sheria na Utii wa Sheria bila shuruti????
Kwa maoni yangu na kwa kuzingatia hali halisi iliyopo kuhusiana na tukio hili, naona yafaa Jeshi la Polisi lingekaa kimya kuhusu tukio hili. Lisingetoa taarifa kama hii ambayo ukiitathmini kwa kina ina walakini na ukakasi mwingi, naona kama inahamasisha Wananchi ili wajichukulie Sheria mikononi.
Polisi hawana mamlaka ya kuhukumu nani ni muhalifu, polisi wanatuhumu tu, mahakama ndiyo inayohukumu.

Kauli hii ya Polisi imefanya makosa ya kutoa hukumu.

Tumeona mifano sehemu nyingi, mfano Amadou Diallo, muhamiaji aliyepigwa risasi na polisi New York City. Amadou Diallo alipigwa risasi akitoa wallet yake mfukoni, pilisi wakafikiri anataka kuwapiga risasi.

Sasa huko Tanzania ambako hakuna uwazi na ufuatiliaji, tutajua vipi wanachosema polisi ndiyo kweli na si cover up?

Ukiunga mkono Polisi kufanya hizi summary execution, jiulize kama tukiruhusu polisi kuua watu hivi, haitawezekana kwa raia wasio na hatia, hata wewe, kuuawa na polisi kwa kubambikiwa tu u panya road na watu wasiokupenda?
 
Hii sio sawa hao polisi siku wakikukuta kona wakasema wewe ni paka road nani atathibitisha ukweli... Japokua uhalifu unakera tusikubali mtego wa kukubali polisi kuua watu. Kutakua na mazishi kila siku.

Uporaji hata mbele upo na watu wanapelekwa mahakamani. Chuma ni pale ambapo hao panya wana silaha (kupambana) sasa hii chuma ya bongo inaonekana polisi hawataki kashikashi za mahakamani so wanatumia shortcut.

N.b siwezi kupendekeza mwanangu mhalifu apigwe risasi ila ashungulikiwe aende jela huko anaweza kutoka huko akawa mtu mzuri.
Word...
 
Kwa hivyo akili za polisi ni km panyaroad wavuta bangi! Wale vijana wanatakiwa wakamatwe wasaidiwe!
Embu sema wewe wasaidiwe vipi?

Kuna tukio limetokea maeneo ya gmboto kuna Dogo amekanyagwa na treni, taarifa zilizopo dogo alikuwa hataki kufanya kazi, wenzake wanampa pikipiki aendeshe hata day waka, mara achomoe kitu kwenye pikipiki, mara anaiba ovyo ovyo anabembelezwa fanya kazi.

Akaenda kuiba mitaa ya tofauti Na kwao, raia kamata piga sana wakamlaza relini treni limepita naye.

Dogo anapelekwa jela anaenda miezi 8, mwaka anarudi anaendelea tena, anarudi tena anaendelea.

Toa wewe ushauri wafanyeje?
 
Sijasupport vijana hao kuuwawa, ila kuwashambulia kwa risasi za mguu ni sawa kabisa kama hawakutaka kujisalimisha na wakaanza kuwashambulia askari, UNLESS HABARI IWE IMEPIKWA.

Taarifa hapo juu inasema waliwataka wajisalimishe ila hawakuwa tayari kufanya hivyo, wakapiga risasi hewanu bado hawakutaka kujisalimisha, mbele ya watu wenye mapanga wanaoshambulia Polisi ilibidi wapambane kwa mikono? Panga unalichukuliaje mkuu?
Watu wanatetea lakini hawatui hao panyaroad wangeondoka na innocent souls gapi kama wasingedhibitiwa kabla hawajafanya
 
Mtoto wako/ndugu yako akiwa mhalifu utakubali apigwe chuma? Au ushabiki maandazi.

Wahalifu washungulikiwe kwa mujibu wa sheria sio kuwajaza hao polisi kichwa waanze kuua watu hovyo! THIS IS NOT A POLICE STATE. Ni nchi ina sheria zake sema ujinga ujinga umetujaa wabongo
Ila jamaa umeelewa maelezo ya police?, ulitaka wakamatwaje wakati walianza kuwashambulia police baada ya kuambiwa wajisalimishe?
 
Back
Top Bottom