Siungi mkono vitendo vyovyote vya uhalifu vinavyofanywa na hao Panya Road, siungi mkono kabisa uhalifu wao ambao wamekuwa wakijihusisha nao.
Aidha, kutokana na rekodi mbaya kabisa za vitendo vya uhalifu na ukiukwaji mbaya wa haki za binadamu ambavyo Polisi wa nchi hii ya Tanzania wamekuwa wakijihusisha navyo, KAMWE siungi mkono vitendo vya hao Polisi kujichukulia Sheria mikononi mwao kama walivyofanya kwa vijana hawa waliouawa. Polisi wa Tz hawana rekodi nzuri ktk kuzingatia Sheria na Haki za watu kwenye utendaji wao wa kazi. Wahalifu sugu hata kwenye nchi zingine za dunia ya kwanza zilizoendelea pia wamekuwa wakishughulikiwa kwa njia kama hizi zilizotumika hapa za kuwaua, malalamiko kutoka kwa umma au wananchi yamekuwa machache sana na wakati mwingine wananchi hawalalamiki dhidi ya Majeshi ya Polisi ktk nchi zao kutokana na sababu kwamba Polisi wao kwa kiasi kikubwa Wana rekodi nzuri ktk masuala ya utii wa sheria zao au kuwa na rekodi nzuri ktk masuala ya kuzingatia haki za binadamu. Polisi wao ni waadilifu, ukiona wameua mtu wananchi wanaelewa wazi kabisa kwamba Polisi wao wamefanya hivyo kwa "nia njema," ili kulinda maslahi mapana zaidi ya umma wa raia wema ktk nchi, wananchi wanakuwa watulivu na wanaridhika kwa sababu wanafahamu kwamba Polisi wamelazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kulinda maslahi yao.
Sasa tujiulize, Je, Polisi wa Tz Wana rekodi nzuri kiasi cha sisi wananchi tuwaamini kwamba watumie njia hii ili kuwadhibiti watu wanaodai kuwa ni wahalifu hatari??? Kutokana na rekodi yao kuwa mbaya sana, Mimi nitakuwa mtu mwisho kuwaamini Polisi wa Tz ktk kutumia njia hii kuwadhibiti wahalifu.