[emoji1][emoji1][emoji1] hujui ni wire au marine board [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bado nina hasira na hawa watu,jamaa wawili walikuwa na boda juzi nilikuwa nafanya mazoezi wakanichapa mgongoni na kitu nahisi ni waya au ubao,wakakimbia sijui lengo lao lilikuwa ni nini...
Mimi nafikiria na kuwaza kwa kutumia Ubongo, huwa siwazi kwa kutumia Makalio kama ulivyo wewe.Kuna mwingine panyaroad kakimbia anaitwa panya white ndio wewe Nini?
Shida ya Watanzania wengi zinaanzia kwenye mifumo yetu ya Elimu iliyopo, watu wengi uwezo wa kufikiri una walakini mkubwa.Polisi hawana mamlaka ya kuhukumu nani ni muhalifu, polisi wanatuhumu tu, mahakama ndiyo inayohukumu.
Kauli hii ya Polisi imefanya makosa ya kutoa hukumu.
Tumeona mifano sehemu nyingi, mfano Amadou Diallo, muhamiaji aliyepigwa risasi na polisi New York City. Amadou Diallo alipigwa risasi akitoa wallet yake mfukoni, pilisi wakafikiri anataka kuwapiga risasi.
Sasa huko Tanzania ambako hakuna uwazi na ufuatikiaji, tutajua vipi wanachosema polisi ndiyo kweli na si cover up?
Ukiunga mkono Polisi kufanya hizi summary execution, jiulize kama tukiruhusu polisi kuua watu hivi, haitawezekana kwa raia wasio na hatia, hata wewe, kuuawa na polisi kwa kubambikiwa tu u panya road na watu wasiokupenda?
Kwani wakati unakwenda Airport unakuwa unatokea wapi?? Nielewe hapo..!! Si kila anayekwenda airport atapita vingunguti na si wote wakiwa wanakwenda airport watapita Nyerere road..!! Hao hao Panya road hawatembei..!!??Vingunguti unayoisema wewe ya uwanja WA ndege kumejaa viwanda na sio makazi ya watu hao panya road wapo vingunguti nnyamani,spenkoni Hadi buguruni huku ndiko sehemu wazazi wanajisifu Kwa wizi wa watoto wao
Kwa taarifa hii ya Polisi, Je, wanatoa ujumbe gani kwa umma hususani kuhusiana na suala la utawala bora wa Sheria na Utii wa Sheria bila shuruti????
Kwa maoni yangu na kwa kuzingatia hali halisi iliyopo kuhusiana na tukio hili, naona yafaa Jeshi la Polisi lingekaa kimya kuhusu tukio hili. Lisingetoa taarifa kama hii ambayo ukiitathmini kwa kina ina walakini na ukakasi mwingi, naona kama inahamasisha Wananchi ili wajichukulie Sheria mikononi.
Shida ya Watanzania wengi zinaanzia kwenye mifumo yetu ya Elimu iliyopo, watu wengi uwezo wa kufikiri una walakini mkubwa.
Nimejaribu kueleza kwa uwazi kuhusu suala hili la Polisi kujichukulia Sheria mikononi kwenye Comment yangu #152, lakini naona watu bado Wana mtazamo hasi juu ya suala la Utawala wa Sheria. Big Chaos!
Sahihi kabisa.Epuken kukaa sehemu ambazo watu wameish apo zaid ya miaka arobain ata kutoka hajawah.
Point muhimu ni kwamba Polisi hawatakiwi kuhukumu nani jambazi na nani si jambazi. Hawana mamlaka ya kusema nani muhalifu na nani si muhalifu.Hao vijana ni wauaji hatari sana Vingunguti, unauliza utawala bora kwa majambazi? Yaani unataka kusema unataka ku negotiate na majambazi? Hivi unacheza wewe na majambazi, polisi wamefanya kazi nzuri sana, dawa ya majambazi ni ku eliminate hakuna njia nyingine, anae ua kwa upanga atauawa kwa upanga, full stop.
Nilichogundua ni kwamba Watanzania wengi wanao support haya mambo wanapenda shortcuts za kijinga ambazo zinagharimu sana.
Wanapenda utawala wa kijeshi, summary executions, madereva wanaokimbiza mabasi etc.
Ukianza kuongea mambo ya due process, rule of law, democracy etc wanakushangaa na kukuona unachelewesha mambo.
Ndiyo maana hata viongozi wa kisiasa wanawachezea sana.
Kuna shida kubwa mahali Fulani kwa wa-Tanzania wengi kuhusu suala zima la kujitambua na elimu ya Utawala Bora wa Sheria.Point muhimu ni kwamba Polisi hawatakiwi kuhukumu nani jambazi na nani si jambazi. Hawana mamlaka ya kusema nani muhalifu na nani si muhalifu.
Hata kuwaita hao watu Panya Road ni makosa, hao ni watuhumiwa bado. Mahakama ndiyo inatoa hukumu na kusema hao ni wahalifu au si wahalifu.
Hiyo ni kazi ya mahakama. Polisi wanatuhumu na kuiachia mahakama Ihukumu.
Sasa, Polisi wakimuua mtuhumiwa, tutajuaje huyo mtuhumiwa ni muhalifu kweli na polisi hawajamuua kimakosa?
Na hata kama ni muhalifu, uhalifu wake ni nini? Na hukumu ya huo uhalifu ni kifo? Na hata kama hukumu ni kifo, polisi ndio wanaotoa hukumu?
Tutajuaje kwamba polisi hawajaua kimakosa watu wasio na hatia (au hata wenye hatia isiyostahiki kifo) na kufanya cover up?
Je, Nani kathibitisha kwamba hao watu kweli ni majambazi??Hao vijana ni wauaji hatari sana Vingunguti, unauliza utawala bora kwa majambazi? Yaani unataka kusema unataka ku negotiate na majambazi? Hivi unacheza wewe na majambazi, polisi wamefanya kazi nzuri sana, dawa ya majambazi ni ku eliminate hakuna njia nyingine, anae ua kwa upanga atauawa kwa upanga, full stop.