Polisi: Vijana wawili waliouawa Vingunguti, Dar ni Panyaroad

Kama ni panya road wamestahili walichokipata,mambo ya utawala bora yaishie huko huko
 
Ngoja niwape hii,. Ukiona mtu ana aka flani hivi ya ajabu ajabu mara nabii mwitu,mara ninja la chuma mara nyingi wana asilimia 70 za uhalifu cc, Paka mwitu
Wangekamatwa wakalime huko jela sio kuua hovyo. Hawa polisi wamepewa mamlaka ya kuua ndo maana wakikuta na vimilioni vyako unakula chuma utasikia tulikua tunamkamata akatuponyoka!
 
Kama kweli ni panya road nawapongeza jeshi la polisi na kuhimiza wananchi wenzangu kuendelea kujichukulia sheria mkononi kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote ile.
 
Ngoja niwape hii,. Ukiona mtu ana aka flani hivi ya ajabu ajabu mara nabii mwitu,mara ninja la chuma mara nyingi wana asilimia 70 za uhalifu cc, Paka mwitu
Kwa kiasi Fulani, Kuna chembechembe Fulani za ukweli kwenye hii hoja yako. Kuna jamaa mmoja ana jina la utani (a.k.a) la "Mkata Umeme," nilipojaribu kuchimbua kiini cha huyo mtu kuitwa kwa jina hilo, nikagundua "mambo mazito sana" juu ya jina lake hili.
 
Vibaka majambazi piga tu chuma za kichwa hamna namna, ukimbembekeza jambaza atakufanya hamna,

Mwendo huo huo mpaka wapotee wote
 
Kama kweli ni panya road nawapongeza jeshi la polisi na kuhimiza wananchi wenzangu kuendelea kujichukulia sheria mkononi kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote ile.
Mtoto wako/ndugu yako akiwa mhalifu utakubali apigwe chuma? Au ushabiki maandazi.

Wahalifu washungulikiwe kwa mujibu wa sheria sio kuwajaza hao polisi kichwa waanze kuua watu hovyo! THIS IS NOT A POLICE STATE. Ni nchi ina sheria zake sema ujinga ujinga umetujaa wabongo
 
Umekula chakula Cha mchana kweli?
 
Nilileta uzi huku juzi kwa namna ambavyo jeshi letu linafanya kazi bila weledi, yaani watu wanamapanga nyie mnawapiga risasi.

Hii inauzi sana
 
Sio mtoto wangu tu, hata mzazi wangu kama ni muhalifu anapaswa kupigwa chuma. Wao wakija kukuibia wanatumia sheria ipi?? au unakaza fuvu tu madam??
 
Nature ya Jeshi letu la Police wakija kukukamata ukiwa na silaha yoyote hata jiwe tu, wanakuua kwanza.
 
Kwa hiyo polisi haiwezi kukamata mhalifu bila kuua? Yaani vijana sita wenye mapanga imekua tabu kukamata au hawataki mambo za mahakamani! Very sad kuambiwa tu fulani panya road just like that afu unakula chuma!
Ndio hivyo, hata wangekuwa na Mawe tu au fimbo bado wangeuliwa tu
 
Kwa hiyo polisi haiwezi kukamata mhalifu bila kuua? Yaani vijana sita wenye mapanga imekua tabu kukamata au hawataki mambo za mahakamani! Very sad kuambiwa tu fulani panya road just like that afu unakula chuma!
Kwa ishu kama hizi polisi hawakosei. Hao hata kama walikamatwa kama kuku chuma lazima wangekula kama polisi Ina uhakika wa matukio Yao. Bila kufanya hivyo vibaka wataendelea kuwasumbua sana
 
Sio mtoto wangu tu, hata mzazi wangu kama ni muhalifu anapaswa kupigwa chuma. Wao wakija kukuibia wanatumia sheria ipi?? au unakaza fuvu tu madam??
Hii sio sawa hao polisi siku wakikukuta kona wakasema wewe ni paka road nani atathibitisha ukweli... Japokua uhalifu unakera tusikubali mtego wa kukubali polisi kuua watu. Kutakua na mazishi kila siku.

Uporaji hata mbele upo na watu wanapelekwa mahakamani. Chuma ni pale ambapo hao panya wana silaha (kupambana) sasa hii chuma ya bongo inaonekana polisi hawataki kashikashi za mahakamani so wanatumia shortcut.

N.b siwezi kupendekeza mwanangu mhalifu apigwe risasi ila ashungulikiwe aende jela huko anaweza kutoka huko akawa mtu mzuri.
 
Vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…