Polisi: Vijana wawili waliouawa Vingunguti, Dar ni Panyaroad

Inasikitisha sana kwa watu wasiokuwa na watetezi bingo,tutaweka wakili haki zao waliodhulumiwa uhai wao,ukiangalia comment ni uthibitisho watu walivo na chuki kwa jamii ambayo sio yao.
Sasa kweli huo muonekano wa huyo jamaa aliyevaa kofia na flana ya njano mpaka upoteze fedha eti unampatia wakili?
 
Kwahiyo kwa maelezo haya ya polisi ni sahihi wamewatoboa macho hao watuhumiwa?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwapiga risasi zilizopelekea vifo vyao Vijana wawili Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) Wakazi wa Vingunguti Jijini Dar es salaam ambapo wamesema Vijana hao walikuwa Wahalifu (Panya Road) na kwamba mwenzao wa tatu bado mwili wake upo Amana Hospital na wenzao wengine wamekimbia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “December 27,2023 lilipokea taarifa kutoka kwa Wananchi wanaochukia uhalifu meneo ya Vingunguti kuwa kuna kundi la Watu vijana akiwemo Panya White kama kiongozi wao wanajiandaa kukufanya matukio ya kihalifu maeneo ya Vingunguti ambapo ufuatiliaji ulianza na Polisi walipofika maeneo ya Vingunguti darajani majira ya saa 2:00 usiku waliwakuta Watu sita wakiwa na silaha za jadi (mapanga) wakiwa wamekusanyika”

“Polisi waliwataka wajisalimishe ili wakamatwe, kinyume chake wakataka kuwashambulia Polisi kwa mapanga, Polisi walijihami na kufyatua risasi hewani lakini mazingira yalivyozidi kuwa ya hatari zaidi Polisi walilazimika kuwajeruhi kwa risasi miguuni na hapo watatu miongoni mwao walifanikiwa kukamatwa huku wakiwa na mapanga matatu yaliyopatikana eneo hilo la tukio”

“Polisi waligundua baadaye kuwa waliokuwa wamejeruhiwa eneo hilo ni pamoja na Paka Pori maarufu Shommy ambaye baadae alijulikana kwa jina la Shomari Salehe Kucheuka na Beka aliyejulikana baadaye kama Bakari Athumani, waliokimbia ni Panya White na mwingine ambaye hajafahamika, hao waliokamatwa baada ya kujeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu lakini baada ya kufikishwa pale Madaktari walibaini kuwa tayari walikuwa wamepoteza maisha”

“Maiti mbili za Shomy na Beka tayari zimetambuliwa na Ndugu zao na maiti moja ya Paka Pori bado ipo Hospitali ya Amana haijatambuliwa na Ndugu na upelelezi wa tukio hili na matukio mengine ya eneo hilo unaendelea”.

Pia soma: Dar es Salaam: Vijana wawili wafariki mikononi mwa polisi

View attachment 2858621

©Millardayo
Huyu mwenye Tshirt ya njano hii namba kabisa🤣
 
Mtoto wako/ndugu yako akiwa mhalifu utakubali apigwe chuma? Au ushabiki maandazi.

Wahalifu washungulikiwe kwa mujibu wa sheria sio kuwajaza hao polisi kichwa waanze kuua watu hovyo! THIS IS NOT A POLICE STATE. Ni nchi ina sheria zake sema ujinga ujinga umetujaa wabongo
Shenzi zako wewe unatetea wezi..hao panya Road uko chamazi walimkata mkono mtoto wa miezi 6
 
Kama ni hivyo hongera zao polisi. Watu kama hao wanaohatarisha usalama wa wa raia, wafinywe tu.
 
Sio mtoto wangu tu, hata mzazi wangu kama ni muhalifu anapaswa kupigwa chuma. Wao wakija kukuibia wanatumia sheria ipi?? au unakaza fuvu tu madam??
Mimi nilishasema mwizi anayetumia siraha huyo ni wa kuua tu hata angekuwa mwanangu
Kuna jamaa huku mwanae alikuwa kibaka akamuonya sana ila mtoto hakusikia ila mama mtu alikuwa anamtetea sana mwanae
Mwisho wa siku mtoto dogo alidakwa mitaa ya bugarika raia tembeza kichapo mpaka dogo akafa baba mtu aligoma kabisa mwili usiletwe kwake dogo alizikwa na manispaa
 
Kwa taarifa hii ya Polisi, Je, wanatoa ujumbe gani kwa umma hususani kuhusiana na suala la utawala bora wa Sheria na Utii wa Sheria bila shuruti????
Kwa maoni yangu na kwa kuzingatia hali halisi iliyopo kuhusiana na tukio hili, naona yafaa Jeshi la Polisi lingekaa kimya kuhusu tukio hili. Lisingetoa taarifa kama hii ambayo ukiitathmini kwa kina ina walakini na ukakasi mwingi, naona kama inahamasisha Wananchi ili wajichukulie Sheria mikononi.
Nalipongeza sana Jeshi la polisi ..Panya road ni majambazi yaliyochangamka kabisa dawa yao ni kuwapelekea maoto kabisa …ni moto tuu!

Kongole Jeshi la Polisi!
 
Mtoto wako/ndugu yako akiwa mhalifu utakubali apigwe chuma? Au ushabiki maandazi.

Wahalifu washungulikiwe kwa mujibu wa sheria sio kuwajaza hao polisi kichwa waanze kuua watu hovyo! THIS IS NOT A POLICE STATE. Ni nchi ina sheria zake sema ujinga ujinga umetujaa wabongo
Acha waue hata kama ni baba , kaka au dada yangu.

Mtu anaeua nae auwawe.

Ubaya tu ni pale mtu anauawa mtu asie na hatia.
 
Inasikitisha sana kwa watu wasiokuwa na watetezi bingo,tutaweka wakili haki zao waliodhulumiwa uhai wao,ukiangalia comment ni uthibitisho watu walivo na chuki kwa jamii ambayo sio yao.
Hawa wajinga wamekula walichopanda chuma chuma chuma chuma 🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫🔫
 
Una uhakika gani hao vijana waliouawa ni panya road ?
Au unaandika usenge tu hapa kimhemuko bila kutumia akili ?
Vibaka na wahalifu mbona tunaishi nao kabisa kwenye jamii zetu na tunawajua kabisa mpaka na wazi wao
Tatizo linakuja huna mamlaka ya kuwawajibisha,na ndiyo maana likitokea gepu kadakwa kwenye wizi wananzengo wanaua tu
 
Nilikuwa na washangaa sana mwanzoni jeshi la polisi eti wanawakamata wanapeleka majambazi mahakamani …..chuma ndio ilikuwa dawa yao
Na nikuhakikishie tu asilimia 95 vibaka wote wanajulikana na polisi tatizo hata wakipelekwa mahakamani ushahidi unakosekana wanaachiwa wanarudi tena uraiani kusumbua
 
Kwa wote:

Back
Top Bottom