Polisi wa Zanzibar kuwakamata watu kisa kuwakuta wakila mchana kipindi cha Ramadhan ni uvunjifu wa sheria za Nchi

Am sure hakuna mahala fulani kuwa ndipo palipo na Mungu Muumbaji wetu,Wala hakuna aliye ama anayemmiliki Mungu. Bali Mungu yupo kwa kila mtu na yupo kwa kila mahala. Wala hayuko kwenye hayo majengo mnayoenda kukutania.
Sema bana watu wenye ngozi ya nguruwe wameshatutawala wametuaminisha kuwa tamaduni zao naa dini zao,chakula Chao,mavazi yao,majina yao ndio mazuri.
Mwili huu ni mavumbi utayaacha hapa Ila roho ipo itaishi milele.
Watu wanafundishana kuwa dini yetu ndio sahihi mbele ya Mwenyezi Mungu, sie ndio tuko sahihi kuliko wale yaani Imani inakuwa Kama ccm vs chadema ama yanga vs Simba.
Dini inatakiwa ionekane kwenye matendo na sio mdomoni mwako.
Dini zinafundisha chuki na kudharauliana kuw wale wanaabudu mizimu,majini, mtu, ng'ombe,yaani unapambania mpaka kufa eti ndio sahihi ama upate tuzo machoni pa watu.
Yaani unafanya matendo kuwaonyesheea wengine kuwa nyie mko sahihi na safi,
Kwa kifupi dini Ni kuwaona yatima ,wagonjwa na wajane.

Sasa wewe jiulize uko dini gani.

Unadhani kuvaa vizuri ukanukia ukaenda huko majumbani mwenu mkakutana na kujazana machuki kichwani na nafsini mwenu Basi mnajua mbingu ya kwenu wenyewe.
Huyo mnayemuabudu sijui aliwambia kuwa mchukiane.
Dini Ni amani na upendo kila dini nzima hata dini yetu waafrika zinahubiri hayohayo
 
Hakuna Sheria Ya Zanzibar Bali Kuna Sheria Ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Na Pia Zanzibar Sio Nchi Ya Kiislamu Wala Kikristu Tutambue Hilo. Ile Sio Nchi Kama Ni Nchi Walete Ushahidi Wa Bendera Ya Zanzibar.
 
Jitahidi sana mkuu kutumia uwezo wako wa kufikiri mbali na uliyoambiwa,ulioona,uliyosikia au uliyosoma.fikiri tu mkuu
 
Si Kila mtu unayemuona mahali Fulani anatokea eneo hilo, mwingine ni mgeni hivyo hana sehemu ya ndani ya kujificha ili apate kula.
ISITOSHE, kufunga ni kutengeneza CONNECTION ya TOBA na MUNGU( Unapopiga mtu kwa kosa la kula unaingia kwenye DHAMBI. Wewe umekula DAKU alfajiri na wakati huyo mtu hajala chochote kutokana na mazingira aliyokuwepo).
SEHEMU kuwa na WAISLAMU asilimia 99 siyo kigezo Cha kupiga watu wanaokula( ni mawazo ya kipumbavu sana). Kama hicho kingekuwa kigezo basi kusingekuwa na misikiti ITALIA, UINGEREZA, UJERUMANI, nk.
NB:
DUNIA hii ni MALI YA MUNGU siyo Mali ya WAISLAMU, na BINADAMU pia ni Mali ya MUNGU na siyo MALI ya WAISLAMU.(Mamlaka ya kumpiga mtu kutokana na kula mnayatoa wapi na wakati hammiliki chochote?, Ikiwa MUNGU MWENYEWE mwenye Mali zake amemwacha huyo mtu aendelee kuzitumia?).
Ni jambo la ajabu sana, mtu mzima unaamua mwenyewe kufunga halafu unaanza kuona wivu unapomuona mtu anakula( Afadhali ungekuwa mtoto mdogo).
Hapo unalimbikiza DHAMBI za HASIRA, CHUKI, KUMDHULU MWINGINE, nk.( Kwahiyo, hao waliopiga mtu ni wahalifu na wakamatwe Kisha washughulikiwe kama wahalifu wengine, tusilee matatizo, yataleta uhasama mkubwa huko mbeleni).
 
Sasa ni waislam gani hao wa Zanzibar wasiojua taratibu za kiislam ?
Hao ni wahuni tu kumbe
 
Sasa ni waislam gani hao wa Zanzibar wasiojua taratibu za kiislam ?
Hao ni wahuni tu kumbe
Hao ni wahuni wasio na elimu na ni watumwa wa mamlaka isiyo na elimu, lakini pia kwa wasio waislam kipindi kama hiki cha mfungo wanatakiwa kufanya matendo ya kutowakwaza waislam kiimani kutokana na majority ya eneo. Yaani mtu asilazimishe kufanya anachojiskia kwenye eneo lenye utamaduni wake kwasababu ya kutegemea yuko huru. Kiufupi tuheshimu jamii ya eneo unapokuwepo kwa kipindi hicho.
 
Kwani kuna ubaya gani mtu ukala ndani kiustaarabu dada angu??
Utanipangiaje pa kulia chakula changu? Kwani ulinisaidia kukitafuta. Walafi tu nyie. Mtu mzima unashindwaje kujizuia na kuendelea na mfungo wako kisa umemuona mtu akila chakula chake? Nyie ni watoto wenye maumbo makubwa tu. Hivyoooo
 
Niujinga kufunga huku unatamani chakula, Tena mtu ulisha kula alfajiri saa 10:50 alafu mchana unaona wivu watu wakila.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
hahaha, kwahiyo unataka tuamini kwamba ISIS, BOKO HARAM na wenzake sio makundi ya kiislam...

pia, ni kweli, Mungu tunayemwabudu sisi, amebagua majini hata kama aliyaumba, hana ushirika nayo, hivyo hayamuabudu, majini kwake ni maasi, yaliasi pamoja na shetani kiongozi wao, LAKINI NINYI MNAYAPENDA NA MNASHIRIKIANA NAYO.

mengine sitaendelea kusumbuana na wewe, hicho ulichoandika hapa watakaosoma ndio watakutathmini na kuijua vizuri dini yako.
 
Kosa la kula hadharani adhabu ni kupigwa bakora?
 
Huna ulijualo.
We waonekana mjazwa chuki ambae huongea kwa naskia hivi naskia vile.
Ushahidi huna.
Kama unataka tukueleze kuhusu ISIS itabidi tukupeleke siasa za mashariki ya kati kipindi US anapanga kufanya regime change Syria.
Najua hayo mambo hauna elimu nayo.

Kuhusu jini nishakueleza,uislam umekataza kushirikiana na viumbe tofauti na wao.
Jini humuabudu Mungu kivyake kwa sababu na yeye jini kaumbwa na Allah.
UWE MUELEWA USIPENDE KULAZIMISHA HOJA.
ALLAH HANA MSHIRIKA BALI ANA WATUMISHI AMBAO NI MALAIKA TULOBAKIA IKIWEMO MAJINI NI WA KUMUABUDU TU.
Laa sivyo lete ushahidi wa uislam kuruhusu kushirikiana na majini.Kuna sheria ya uislam na kuna hurka ya mtu.Hao wafanyao hivyo ni hurka zao uislam sheria haijaruhusu.
Kwahiyo wataka kusema Mungu wenu mbaguzi?
Alivuja damu msalabani kisa mliomkosea ila kiumbe cha jini kakibagua??
Basi Mungu wako hajakamilika hana tofauti na binadamu.
Kwa sisi waislam Jini ni kiumbe ila shetani ni tabia.Ila jini aliyeasi mkuu aliitwa Ibilisi.
Hivyo Jini anamuabudu tu Mungu ila hashirikiani na yeyote isipokua majini wenzake.
MUngu watumishi wake ni Malaika tu.

Acha alfulela hulela uwe na ushahidi na unalozungumza laa sivyo utakula za uso kila siku.
 
Hivi uislam unakufundisha ubaguzi kiasi hiki? Zama za ubaguzi zilishapitwa na wakati na hutofanikiwa.
Mungu anawapenda wote, iweje wewe binadamu tu?
By the way Zanzibar aiongozwi kidini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…