Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti


Inawezekana ACP Mambosasa ni polisi wa Rwanda na ACP Mussa ndiyo polisi wa Tanzania....

Kwanini polisi wa nchi moja tena wakiwa wanaongoza mkoa mmoja wawe na kauli za kutofautiana juu ya tukio moja la uhalifu lililotokea ndani ya eneo lao la kiutawala???

Tuseme nini sasa? Kwamba, serikali ina kikundi cha askari cha utekaji wa watu wakosiaji wa utawala huu huku baadhi ya viongozi wakuu wa polisi wakiwa hawajui??

For sure, kauli hizi mbili zinazokinzana za viongozi wakubwa wawili wa polisi ndani ya mkoa mmoja, nchi moja zinathibitisha kuwa utekaji wote wa critics wa serikali, kushambuliwa kwa risasi kwa watu kama Tundu Lissu na uhalifu wote unaofanana na huu, unatekelezwa na dola chini ya uratibu wa ikulu....!!
 
Guys you know what?? Once the IGP tries to get his hands on Mambosasa and gets hold of him, this will be the end of his tenure in the office. With all my due respect for the IGP, I suppose you execute what is lingering in your mind and have it done once and for all.
 
Tukio kubwa la kipolisi lililotokea siku nne zilizopita lililotikisa dunia nzima polisi mkoa mzima wa Dar wasijue ikiwa ni pamoja na IGP? Lingetokea Katavi ingechukua miaka mingapi lifike Makao Makuu ya polisi? Kama hali ndo hiyo, madai ya polisi kuwa uhalifu nchini umepungua si kweli bali ni taarifa tu za uhalifu toka mikoani hazijamfikia msemaji mkuu wa polisi.
 
Hakuna cha tukio kubwa hapo acheni kukuza mambo. Huyo Tito kakamatwa kama watu wengine wanavyokamatwa. Hana ukubwa wowote hadi eti useme tukio kubwa. Kitu kingine lazima ufahamu kuwa polisi wana taratibu zao za kutoa taarifa. Hawaropoki ropoki tu kama nyie mnavyotaka iwe. Na kitu kingine hakuna anayejua upande wa pili wa maisha ya Tito, msimfanye aonekane msafi wakati mmejulia tu kwenye twitter na kwenye maisha yake ya sheria.
 

Duuuuu, kwahiyo hapo umemaliza utetezi. Basi shughuli ipo.
 
msipende kuzua taharuki za kishamba, mamboleo kasema alikamatiwa kinondoni na sio polisi wa kinondoni waliomkamata tatizo nini?
Naona unataka kupindisha ,mamboleo anasema amekamatwa na polisi na yupo ktk mikono salama.
 
Tumekuwa wapumbavu. Hawa wauaji kila siku wanadonoa mmoja baada ya mwingine. Na sisi kwa ujinga tunaona kama yanayotokea hayatuhusu.

Ningependa kusikia kipaumbele cha kwanza cha vyama vya siasa, makanisa, misikitiki, vyama vya kiraia na taasisi za kimataifa, ni kuongoza mapambano dhidi ya wasiojulikana/watekaji na wauaji.
 
Jiwe anaogopeka mkuu
 
Habari ya Tito na wengine wanaotekwa na kupotea inaweza kufanana na huyu Mwandishi

Mahakama moja nchini Saudi Arabia imewahukumu watu watano kifo na kuwafunga wengine watatu baada ya kuwakuta na hatia ya mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi mwaka jana

Khashoggi, alikuwa mkosoaji kinara wa serikali ya kifalme ya Saudia aliuawa ndani ya ofisi ndogo ya ubalozi wa nchi hiyo katika Jiji la Istanbul, Uturuki mwaka 2018.


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Saudia amesema mauaji hayo yalikuwa ni sehemu ya "operesheni haramu" na kuwashtaki watu 11 ambao hata hivyo majina yao hayakuwekwa wazi.

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa (UN) alifikia hitimisho kuwa yalikuwa "mauaji ya serikali yasiyofuata utaratibu."

Mtaalamu huyo Agnes Callamard pia alipendekeza kwenye ripoti yake kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman achunguzwe kutokana na mauaji hayo.

Bin Salman hata hivyo amekanusha kuhusika kwa namna yeyote ile, lakini mwezi Oktob mwaka huu akasema kuwa "anawajibika moja kwa moja akiwa kama kiongozi wa Saudia, na hususani kwa kuwa mauaji hayo yametekelezwa na maafisa wa serikali ya Saudia."

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kesi hiyo haikukidhi viwango vya kimataifa na mamlaka za nchi hiyo "zilizuia njia zote stahili za uwajibikaji".

Mwandishi huyo aliyekuwa na miaka 59 alipofikwa na umauti alikuwa akiishi Marekani na kuandika maoni kwenye gazeti maarufu la Washington Post.

Mara ya mwisho kounekana akiwa hai ilikuwa Oktoba 2, 2018 akiingia kwenye ofisi ndogo za ubalozi wa Saudia ili kuchukua karatasi zake za talaka.

Alikuwa mbioni kumuoa mpezi wake wa Kituruki Hatice Cengiz.

Baada ya kusikiliza kanda za sauti zilizonaswa na maafisa wa usalama wa taifa wa Uturuki, Bi Callamard alifikia hitimisho kuwa Khashoggi "aliuawa kinyama" siku hiyo.

Naibu mwendesha mashtaka wa Saudia Shalaan Shalaan aliwaambia wanahabari Novemba 2018 kuwa mauaji yaliamriwa na mkuu wa "timu ya mapatano" iliyotumwa Istanbul na mkuu msaidizi wa idara ya usalama wa taifa ya Saudia kwa kazi ya kumrejesha Khashoggi nyumbani "kwa jia ya ushawisi" na edapo hilo lingeshindikana, "basi kwa nguvu".

Wachunguzi pia walifikia hitimisho kuwa Khashoggi alifungwa kwa lazima ma kisha kukabwa koo na kamba kabla ya kudungwa sindano lukuki za dawa ambazo zilipekea kifo chake. kwa mujibu wa bw Shalaan.

Baada ya hapo mwili wake ulikatwa katwa vipande na kukabidhiwa kwa mshirika wa kituruki nje ya ubalozi. Mabaki hayo hayajapatikana tena.

Bw Shalaan hata hivyo anasisitiza kuwa Mwanamfalme Mohammed "hakuwa na habari yeyote juu ya tukio hilo".
Siku wasiojulikana watakapojulikana nao watanyongwa tu...
 
Muhimu umefahamu ujumbe, spellings za lugha ya watu weka pembeni..

Anyway unajua kama unaweza kuandika COLOR na COLOUR na maana ikawa ndio ile ile
Unatetea makosa ya uandishi au?
 
Hii movie musa taibu atakuwa hajashirikishwa, na mamboleo kapewa taarifa juu kwa juu
 
Nilivyomuelewa kamanda wa kinondoni ni kwamba yeye kama yeye kwenye mkoa wake hajamshika Tito ila kuna Operation zinawezwa kufanywa na mkuu wa kanda nzima na yeye asipewa taarifa kwa mantiki hiyo Mambosasa na BASHITE ndio wamemkamata Tito/Bolleni ukiunganisha nukta.
 
Huyo Bashite Ni Nani katika jeshi la polisi? Sirro sio pilato haogopi makelele
 
Nyaraka gani Hizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii imedukuliwa na wasiojulikana,wanafanya kazi zao mchana ila hawafahamiki,wanatumia vyombo vya moto(magari/pikipiki) ila hawakutani na msongamano wala traffic.
Hatuna bahati wala usalama kama wananchi na hakuna MTU kuwajibika.Kila mmoja anatoka na blah blah zake halafu kimya totoro.
Tuchukue hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…