Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti

Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni asema hana taarifa za kukamatwa na kushikiliwa kwa mwanaharakati,Tito Magoti

Mussa Taibu amesema kuwa mpaka sasa hana taarifa ya kukamatwa kwa Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC] Tito Magoti, katika eneo la himaya yake na hata amejaribu kuwauliza wenzake lakini nao hawana taarifa hizo.

Awali Kamanda Lazaro Mambosasa aliuthibitisha Umma kwamba Magoti alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni

Taarifa za awali kuhusu kutekwa kwa Tito Magoti ni kuwa alikuwa katika bodaboda akielekea Mwenge kununua simu, alipofika katika kituo cha mafuta cha Puma watu 5 waliokuwa na gari aina ya Harrier walimchukua kwa mabavu kisha kuondoka kwa uelekeo wa Posta, Dar es Salaam.

Jana Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar, Lazaro Mambosasa amekaririwa akisema Polisi inamshikiliwa Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia.

Hata hivyo, Mambosasa hajawahi kubainisha ni kituo gani ambacho Magoti anashikiliwa.

Zaidi, soma:

View attachment 1301209
View attachment 1301208
Waandishi wa habari mnashindwa wapi?
Aliyesema Magoti yuko mikono salama kwani anaishi mbinguni? Kwanini muende Kinondoni badala ya kumganda Mambosasa aseme Magoti yuko wapi au kituo kipi? Kwanini mnazunguka zunguka?
 
Jeshi la polisi lilimkamata Tito Magoti kwa madai eti anatumia fake I'd kuitukana serikali huku wakimhusisha na Kigogo wa Twitter pamoja na I'd ya member maarufu mkosoaji wa Jf...Cha ajabu watu waliohusishwa naye bado wapo wanapost tu...Leo wanasema hawajui alipo ili baadaye wakamtelekeze sehemu kama walivyofanya kwa Mo baada ya kumsainisha nyaraka muhimu kwa nguvu.
Nyaraka gani hizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi la polisi lilimkamata Tito Magoti kwa madai eti anatumia fake I'd kuitukana serikali huku wakimhusisha na Kigogo wa Twitter pamoja na I'd ya member maarufu mkosoaji wa Jf...Cha ajabu watu waliohusishwa naye bado wapo wanapost tu...Leo wanasema hawajui alipo ili baadaye wakamtelekeze sehemu kama walivyofanya kwa Mo baada ya kumsainisha nyaraka muhimu kwa nguvu.
Wameshampa kipigo cha mbwa koko, Magoti yuko mahututi, Polisi wanaogopa kumtoa hadharani...
 
Mpaka tutekwe wote ndio tutajua umuhimu wa kuungana kama Taifa kupinga huu udhalimu.

Naanza kupata mashaka kama Tito bado tunae na kama tunae,basi sijui atakuwa katika hali gani.

Ukiona hivi, uje kuna mawawili:wamemtanguliza au wamemuumiza na kumjeruhi vibaya kiasi kwamba hawako tayari kuhusishwa/kutuhumiwa na hivyo tunaweza kumuokota akiwa kama Dr.Ulimboka.

Una akili sana..
 
Really? Wabongo kwa kupenda uongo. Yani maoni yako unataka kubadili ni kweli!
Mkuu, jifunze kuandika kiswahili, unatakiwa ufahamu huo ndio ukweli katika nchi yetu..

Ukisikia mtu anahojiwa ujue anakula KICHAPO , Ukisikia mtu ana fanyiwa INTERROGATION ujue ana fanyiwa TORTURE

We are animals, that's what we are,...
 
Waandishi wa habari mnashindwa wapi?
Aliyesema Magoti yuko mikono salama kwani anaishi mbinguni? Kwanini muende Kinondoni badala ya kumganda Mambosasa aseme Magoti yuko wapi au kituo kipi? Kwanini mnazunguka zunguka?

Waandishi wa bahasha, utashangaa wamesikiliza halafu hakuna swali.
 
Duh....

Hii ni hatari sana......

Wanawezaje hivi sasa kukanusha, wakati hapo nyuma waliikiri kuwa wao ndiyo wanaomshikilia huyo Tito Magoti?

Huu ni ushahidi wa mazingira kuwa wao Polisi, kumbe ndiyo wale watu tunaofahamishwa kuwa ni watu WASIOJULIKANA!
msipende kuzua taharuki za kishamba, mamboleo kasema alikamatiwa kinondoni na sio polisi wa kinondoni waliomkamata tatizo nini?
 
It might be katika kumtesa aseme wanayotaka kuyasikia amekufa sasa inabidi watafute namna ya kujinasua!
 
Swali la kujiuliza kabla ya kuanza kumlaumu nani au yupi kafanya nini ni hili "Kwanini waandishi wa habari wamemuuliza swali mtu mwingine ambaye hakuhusika na taarifa za kukamatwa kwa mhusika?
Nashauri kabla ya kuanza kulaumu yeyote,ni vema LHRC/mwajili wa mhusika kwa pamoja na ndugu wa familia wakafuatulia taarifa rasmi kwa mhusika aliyetoa taarifa za awali kuwa wanamshikilia mhusika anayedaiwa kupotea.
 
Back
Top Bottom