Katika nchi yoyote inapojitafutia haki inatafuta mtu mmoja tu awe chanzo, Damu yake inaweza ikalia juu ya nchi na kuanzisha mambo ambayo kila mtu akajiuliza mbona yamekuwa aya yote na madhara yake yanaweza yakawa ya mda mrefu......Soma vitabu vya dini... inasema BINADAMU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.
Lazima muelewe kuwa chanzo cha Taifa lolote ni nafsi ya kila mtu mmoja mmoja, maana lolote katika nchi uanza na mtu mmoja Tu na viongozi wengi wasio na hekima huzarau kwa kufikiri kuwa ni mtu mmoja tu ana madhara. Ukisoma vitabu vya dini vinasema HAKI huanza kwa mtu mmoja tu...
Kumbukeni mungu akuitaji jeshi kuwakomboa wana wa israel wapate HAKI YAO ila alimuitaji MUSA tu kuwakomboa wana wa israel. Najua wengine mnaweza kudharau na kuuliza yeye ni nani? mkumbuke biblia mungu alimuinua musa sehemu ambayo ajulikana na kumfanya taifa.
Mkumbuke taifa lolote ni mtu mmoja tu biblia inasema alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mtu mmoja nao wakae katika nchi, nataka muelewe Taifa chanzo chake ni mtu mmoja TU.. Kwa iyo chochote kinachozaanzishwa katika taifa inaitaji moyo wa MTU mmoja Tu kinawe kuzua jambo kubwa sana
Vitabu vya dini vyewewe kuanzia mwanzo mpaka mwisho katika kila jambo ambalo lilitokea lilianzia kwa mtu mmoja tu.. viongozi wanapaswa kutibu ndani na nje patatibika, mkumbuke farao na jeuri yake yote MUNGU alimuonyesha yeye ni mungu wa viumbe wote, Jifunzeni sana hekima mnapokuwa viongozi kwa maana panapo kibuli huja HASARA katika NCHI NDO VITABU VYA DINI VINAVYOSEMA.
MKUMBUKE HUKUMU YA YESU KATIKA BIBLIA
"Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo? Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda. Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.