Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

Nguvu uhitajika kwenye kufanya kosa la kihalifu tu, lakini kwenye jambo la kheri, upendo tu unatosha. Kulikuwa na ulazima gani kwenda kufanya fujo kwa watu? Na hadi kuteka mtoto dah!

Apumzike kwa amani.

.Ova
 
Yaani Polisi nao wakashiriki kumshambulia huyo jamaa mpaka kumuua?....hata hao hawaitii Sheria?
 
Huyo mtoto ni WA mashemeji zake ambazo nao walikuwa wanampinga
Igeuze hivi:
Dada yako agombane na mume wake, baada ya ugomvi wao, dada yako anaondoka na mtoto kwenda kwa wazazi wenu.
Halafu huko ulipo unaletewa taarifa kwamba baada ya dada yako kugoma kumpatia mume wake mtoto wao, mume huyo kaamua kubeba mtoto wako na kuondoka naye.
Wewe ungeipokeaji hiyo taarifa ? Na unadhani ungemfanyaje huyo shemeji yako?
 
Polisi gani hao wanashambulia watuhumiwa kwa mapanga badala ya kumkamata na kumpiga pingu ukilinganisha wapo wengi?

Huyo jamaa hana akili vilevile. Unachukuaje mtoto usiyemjua ili urudishiwe mwanao?

Sehemu nyingine za hii nchi bado zipo nyuma kwa viwango vya kutisha. Hii story nzima unaweza dhani ni brainless comedy.
 
Kuna matukio yakitokea yanafikirisha na kudhihirisha uwezo mdogo sana walionao baadhi ya watu/jamii fulani wa kuchanganua mambo (Mema na Mabaya) ya kufanya na ya kutokufanya.

Azikwe, halafu waliobaki hai waowaji na waolewaji walogane au wauane.
Ili mpate matukio ya kutusimulia tena.
 
Mkuu, mahari inadaiwa wapi
 
Polisi wajitafakari, hizi chuki wanazotengeneza zikiendelea baina yao na raia kuna siku raia watakosa uvumilivu halafu waanze kutafutana.
Hapo hakuna chuki. Bali ni kuwa unprofessional. Obviously hawakujua cha kufanya juu ya situation kama hiyo au jinsi ya kudeal na mtuhumiwa aggressive zaidi ya kupigana mapanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…