Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
Haya umeshiba tayari nenda ukanye.

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
 
Mbona wapenzi wa soka wanasongamana kwenye viwanja vya mpira?

Unataka kutuambia kuwa kwenye hatari ya corona ni kwenye makongamano ya Katiba ya chama cha Chadema pekee??
Ndio maana wakasema mikusanyiko ya lazima na isiyo ya lazima! Ya lazima cautions zimeanza kuchukuliwa, ikiwemo na kuvaa barakoa kila mtu na social distancing, isiyo ya lazima kwa sasa (eg makongamano) can wait! Nyinyi si ndiyo mlikuwa mnacomplain serikali ya Magu haichukui hatua dhidi ya corona? Now zimeanza kuchukuliwa mnazipinga tena?
 
Mandela alikuwa gaidi kwa mtizamo wa Kaburu.
Kwani siasa ya kibaguzi iliokuwa inatekelezwa na makaburu ilimfanya Mandela aende nje kujifunza mikakati ya kijeshi ili kupambana na walowezi hao.
Na kweli aliporudi walianza kulipua miundo mbinu kama vituo vya umeme nakadhalika hadi alipokamatwa na kufungwa kifungo cha maisha.
 
Japo hatujui undani wa tuhuma zinazomkabili Mbowe lakini kuna uwezekano mkubwa Mama ameamua kumtungua kabla hajatua.Mbowe angevuta subira huku akiusoma upepo na labda tungevuna mbivu.Ila kwa sasa Mama kawa mbogo hataki kudharauliwa au kupangiwa afanye lipi na aache lipi She is Command in Chef.
 
Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
Utoto na upuuzi ndiyo unakusumbua.
 
Tatizo, anatuma wa shauri wa Magufuli kuendesha nchi.
 
CCM imechanganyikiwa, haijui ifanye lipi. Walitaka kurejesha haki, wajakuta uwezo wa kuwashawishi wa Tz kwa haki hawana mana hawana ushawishi wa kutosha, hivyo wanarudia tens kulekule kwa kutumia majeshi na kubambika kesi ili waendelee kuwa madarakani.
Bila majeshi CCM haina uwezo tena kushika hatamu za uongozi wa watz.
 
Toka nchi hii ipate uhuru kuna kesi kama mbili ama tatu za Uhaini. Lakini toka tumepata kuanza mfumo wa vyama vingi vya kisiasa kumekuwepo na kamatakamata hasa kule ambapo Samia katoka Zanzibar kutokana na mfumo wao wa Siasa za chuki.

Magufuli alikuwa mhuni tu na ukatili wake wa kumalizana kikatili kisiasa kwa Wapinzani wake uongozi wake uliweza kutumia mfumo wa kueliminate Wapinzani mfano hai ni tukio la Lissu. Pamoja na mambo yake kidogo alikuwa na haya ama aibu kwa kuogopa kuonekana mbele ya jamii ya wastaarabu ukatili wake kukaundwa msemo wa watu wasiojulikana.

Huyu mama sijui anatafuta nini ama haelewi kuwa kapachikwa pasi moja mbaya sana kutokana na kusifiwa kuwa anaupiga mwingi sasa kapewa pasi mkasi kwa kumpa Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzania kesi ya Ugaidi. Mama ajue kabisa kajitafutie ubaya na waliokuwa wanampenda.

Hofu yake ni nini kwani angeacha haya makongamano ya kudai katiba mpya angepungukiwa na nini? Kenya wanaupinzani Mkubwa na kufikia hatua ya Mpinzani kujiapisha kuwa Rais wa watu wa Kenya hatukusikia Ugaidi wala Uhaini.

Mama nakutabiria utaongoza hii nchi kwa hofu kubwa sana. Tegua huu mtego ambao wapinzani wako ndani ya CCM hasa akina Mwigulu wanakupigia ngoma unaicheza.

Zipa masikio acha kukanyaga Katiba ruhusu watu waongee. Wewe ni mama unajisikiaje mtoto wa mwanamke mwenzio anasokomezwa kesi ngumu kuwa na huruma.
 
Subiri afike mahakamani haki itapatikana huko msitake Rais aingilie mhimili mingine pamoja na utendaji kazi wa idara zake.

Katoka Mdude

Wametoka Mashehe

Seti yupo nje

Hata Mbowe atatoka kama hakuwa na hatia.

Huo ndio utawala wa sheria.
 
Hivi hatuoni aibu kuiita CHADEMA chama kikuu cha upinzani? Ukuu wake uko wapi wakati kina mbunge mmoja tu? wa Nkasi kaskazini. Nani kawafunga akili nyie mazuzu? Si bora ungeiita ACT-Wazalendo chama kikuu cha upinzani maana kina wabunge wengi kuliko CHADEMA. Bado tu hamuamini chama chenu ni sawa na TLP na NCCR-MAGEUZI kwa tofauti ya kuwa na mbunge moja tu?
 
Amewekwa kati na manyang'au, hachomoki huyu. Labda ajivue ufahamu, hiyo ndio itakuwa salama yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…