Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Kalipe vitu vya watu...yaani Dunia hii unaokota simu Tena smart unaanza tu kutumia .... Kudadeki .......kalipe Mzee.
Tena huyo kesho anaweza kuja humu na akatuambia kua kaokota nyumba!! Vijana wa siku akili zao wanazijua wenyewe!!
 
Zima simu hiyo kisha sepa ukienda police wakakupiga sana ukute hao walio iba vitu vya jamaaa .....hasa ukiwa una muonekano wa kiteja teja watakuua kabisa
 
Kama kesi ya wizi tu utakuwa na bahati sana
Sasa unaokota simu unaitumia ukiambiwa alieibiwa aliuwawa pia utatokaje hapo?
Simu sio ya kuokota wewe hiyo ina kesi kubwa
 
Ukiokota simu sheria inasema iwasilishe kituo chochote cha polisi, wao watamtafuta mwenye nayo.
 
wabongo kwa kweli bado sana, hakuna kitu cha kuokota, unapookota unatakiwa umtafute mwenyewe umkabidhi mali yake na sio kujimilikisha, huo ni sawa na wizi.
 
Kwani ulivopigiwa umeulizwa details zako kama jina au nini? Toa line na ui flash isibaki na habari zozote kukuhusu ukaitelekeze kituo cha police kama una ujasiri lakini
 
Watakapokuminya kende lako moja, utasema ukweli wako wote! Bila shaka simu yenyewe ndiyo hii unayochat nayo humu JF?!
 
Safisha mstari maringo vizur kabla hujaenda kuripot
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…