Umenikumbusha nilipokuwa Sumbawanga kikazi mwaka 1987 niliokota pochi ya mfukoni nzuri sana imetengenezwa kwa ngozi ya mamba, kwa wanaozijua wanazielewa na zina bei kali. Pochi hiyo ilikuwa nzito kiasi, kutokana na desturi zangu tangu utotoni sikutaka kuifingua, niliipeleka kituo cha polisi na nikaikabidhi kaunta, ilipokelewa na askari akaifungua mbele yangu, cha ajabu yule askari aliondoka haraka kimya bila kusema neno. Nilisimama kaunta kwa dakika 15 hivi bila kumuona akirudi, nikaamua kuchungulia mna nini ndani ya pochi. Kumbe pochi ilikuwa na vijitambaa vyeusi bilivyoviringishwa na kufungwa, nikahisi ni hirizi.
Alikuja askari mwingine nadhani aliingia zamu akaniuliza ninachosubili nikamueleza na kumuonesha ile pochi, naye akachungulia kilicho ndani, cha ajabu naye akanyata taratibu kimyakimya, hakurudi! Nilipoona hivyo nikaamua kuichukua na kuondoka nayo. Nilipofika nyumbani nikaamua kuchukua koleo ya fundi umeme nikavivuta vile vidubwasha na hamadi! Chakuokota si cha kuiba chini yake kulikuwa na shs. 674,500/= na kwacha 55,000/= za Zambia, nikajisemea moyoni Mingu anipe nini, alhamdulilah.