Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Huyo mamako alikudanganya. Alienda kudanga akahongwa hiyo simu na mwizi au jambazi, muulize vizuri.

Babako unamjuwa? Mnaishi nae?
Dah umemkosea sana huyo jamaa.

Leo nimeconfirm kichwani ni mtupu hadi sio poa.
 
Naona watu wengi mna mbishia mwanba kuhusu kuokota simu..
.
Wew kama huna bahati ya kuokota sim usisem haiwezekani kuokota simu
.
M mara mbili nishaokota simu
Mara ya kwanza naingia dukani kwa mangi nakuta kwa nje kuna sim imedondoshwa na namuliza muuzaji anasema hajui sema nikamua tu kumpa muuzaji kama mwenye sim akitokea ampe lkn sjh kama kwel alimpa au alibaki nayo mwenye.
.
Sim ya pili nashuka kwenye bajaji na na m ndo abilia wa mwisho. Ile kushuka tu naangalia kwenye kiti kama kuna sarafu nimeangusha naona samsung moja imenyooka sana. Nikasema hii nikimpa bajaji sizan kama mwenye sim anaweza mpkata bajaji so hii nikamuoa kutoa lain nikakaa nayo kama wiki hivi nikaona niuze.

Lkn pia nishaokota sim ofcn kwangu. Hii ilikuwa samsung fold mpyaa tena enzi zile zintoka sema hii sikuzima wala nn nikaweka kwenye droo baada ya mda kupita akaja mzee mmoja nilimuhudumiaga akauliza kama alidondosha nikamwambi nilikutunzia hii hapa.
.
Kuokota sim kupo ila kama hujawah kuokota usimseme jamaa cha msingi hapo mshaulini tu namna gani anatoboa kama hakuiba kweli...
Mkuu kuokota simu kupo, ila ni vyema ukaiacha hewani ili mwenye nayo akipiga upate kumrudishia. Huu ndio ubinadamu.
 
hio haisaidii simu wanatrack kupitia IMEI namba hivyo laini yoyote utakayoweka inaleta taarifa zako na huyu mleta mada aliweka laini yake tayari system imemtambua hasa kama laini aliyoweka alisajili kwa NIDA yake ndio kabisa hana ujanja
Simu naitupa kabisa,natumia simu yenye imei nyingine na laini nyingine kabisa,hapo vipi mkuu?
 
Sure. Kimasihara sana jamaa anaenda jela.

Hii ni sehemu ya kula ya polisi.
Hapo wanaweza kumpa kesi ya mauaji. Yaani watasema mwenye simu hii aliuawa. Ukiiona simu popote pale kimbia spidi zote maana huo ni msala.
 
Ulitakiwa ukaripoti polisi kuwa umeokota simu ..
 
Ukiokota simu peleka polisi au tangaza gazetini.

Kwanza hata usitangaze, unaweza kuokota kitu kinachoonekana simu kumbe ni bomu la kujilipua lenyewe kama huko Lebanon.
Siku moja gari la Magereza lilipita spiidi ikadondoka kofia ya afisa magereza. Nikapeleka kituo cha polisi. Yaani pamoja na wema niliofanya niliulizwa maswali mengi sana. Moja ya maswali waliniuliza.
" Kofia kama hii kwanini umeileta polisi kwanini usiiache hapo hapo?"
Swali la kimtego nikawajibu kwamba Kofia hii ina nembo halisi ya jeshi la polisi magereza, kama mhalifu ataipata kazi yake itakuwa ndogo sana ni kujishonea mag Wanda na akikamilisha ataenda gereza lolote na kujifanya askari akafanya uhalifu wowote.
Huwezi amini niliachiwa nikarudi nyumbani. Kesho yake nilipoenda kuripoti nikaambiwa jamaa alienda kituoni kuulizia kama kuna kofia imepelekwa pale. Niliikuta elfu kumi zawadi.
 
Sasa nawewe kwan ulihangaika hivyo? Mimi wangenikuta ndo nakojolea wakati wanarudi kuitafuta
 
Kuokota simu si jambo la ajabu. Nashangaa watu wanashangaa. Wangapi wanadondosha simu kila siku? Halafu nmesikitika sana kuna mmama mtu mzima ambaye huwa anajinasibisha kuwa mtu wa hekima na dini ameandika ujinga kuhusu mama wa mhanga huyu wa simu. Inasikitisha mwanamke kumtusi mama wa mtu ambaye ni mwanamke mwenzake tena tusi kubwa eti amedanga amehongwa. Wewe Bibi jifunze kuheshimu watu. Haikupunguzii kitu.
Kuna demu ni rafiki yangu alidondosha simu iPhone kwenye bajaj za ukonga banana kutoka mjini nadhani. Ameshuka ktk bajaj anatembea mwendo wa dakika kama tatu akagundua hana simu anarudi kituoni huku akiangalia labda kaidondosha on the way lakini hola. Ikabidi akubali matokeo. Kufika home akachukua simu nyingine kupiga Ile namba. Simu imeita kama mara tatu haikupokelewa. Baada ya nusu saa akapiga tena, Mzee mmoja akapokea akaniambia wakati anashuka na alikuwa wa mwisho ktk bajaj akasikia mlio wa sms kuingia ktk simu ndo akaona simu akachukua. So kwakuwa anaishi mbali Kivule ndani ndani uko na keshafika home kesho wawasiliane. Yule Mzee akasema na naona haina charge itazima akachukua namba ya yule dada. Kweli kesho yake anapata simu yake. Haya mambo yapo.
Shida ni huyu jamaa mhanga wa simu kuanza kutumia yeye Bora angeenda kuuza kwa mafundi simu wao ili kupata spea za simu zingine mbovu. Ndo watu wanafanya siku hizi hata wezi wa simu hauzi kwa mtu jau siku hizi unaweza kulewa kesi za mauaji kizembe.
Anaeokota simu ndio kama huyo anamrudishia mwenyewe au anaisalimisha polisi. Huyu anaeokota na kuanza kuitumia ni mwizi na akitaka kujua akaripoti polisivwanakomuhitaji aende.
 
Umenikumbusha nilipokuwa Sumbawanga kikazi mwaka 1987 niliokota pochi ya mfukoni nzuri sana imetengenezwa kwa ngozi ya mamba, kwa wanaozijua wanazielewa na zina bei kali. Pochi hiyo ilikuwa nzito kiasi, kutokana na desturi zangu tangu utotoni sikutaka kuifingua, niliipeleka kituo cha polisi na nikaikabidhi kaunta, ilipokelewa na askari akaifungua mbele yangu, cha ajabu yule askari aliondoka haraka kimya bila kusema neno. Nilisimama kaunta kwa dakika 15 hivi bila kumuona akirudi, nikaamua kuchungulia mna nini ndani ya pochi. Kumbe pochi ilikuwa na vijitambaa vyeusi bilivyoviringishwa na kufungwa, nikahisi ni hirizi.
Alikuja askari mwingine nadhani aliingia zamu akaniuliza ninachosubili nikamueleza na kumuonesha ile pochi, naye akachungulia kilicho ndani, cha ajabu naye akanyata taratibu kimyakimya, hakurudi! Nilipoona hivyo nikaamua kuichukua na kuondoka nayo. Nilipofika nyumbani nikaamua kuchukua koleo ya fundi umeme nikavivuta vile vidubwasha na hamadi! Chakuokota si cha kuiba chini yake kulikuwa na shs. 674,500/= na kwacha 55,000/= za Zambia, nikajisemea moyoni Mingu anipe nini, alhamdulilah.
Hiyo pochi ya mfukoni au ya begani?
Maana kwa fedha hiyo kapochi kulikuwa kakubwa bila shaka
 
Siku moja gari la Magereza lilipita spiidi ikadondoka kofia ya afisa magereza. Nikapeleka kituo cha polisi. Yaani pamoja na wema niliofanya niliulizwa maswali mengi sana. Moja ya maswali waliniuliza.
" Kofia kama hii kwanini umeileta polisi kwanini usiiache hapo hapo?"
Swali la kimtego nikawajibu kwamba Kofia hii ina nembo halisi ya jeshi la polisi magereza, kama mhalifu ataipata kazi yake itakuwa ndogo sana ni kujishonea mag Wanda na akikamilisha ataenda gereza lolote na kujifanya askari akafanya uhalifu wowote.
Huwezi amini niliachiwa nikarudi nyumbani. Kesho yake nilipoenda kuripoti nikaambiwa jamaa alienda kituoni kuulizia kama kuna kofia imepelekwa pale. Niliikuta elfu kumi zawadi.
Kuna jamaa na yeye alikutana na binti anazurulazurula na nguo za shule (primary) kama km 20 nje ya mji.Kumuuliza binti haelewi.Akamlipia nauli akampeleka kituo cha polisi.Kwa kifupi jamaa alikoma sidhani kama atarudia tena.
 
Back
Top Bottom