Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Ukiokota simu peleka polisi au tangaza gazetini.

Kwanza hata usitangaze, unaweza kuokota kitu kinachoonekana simu kumbe ni bomu la kujilipua lenyewe kama huko Lebanon.
 
Mambo kdg namna hio unaogopa, huo sm tupilia kule Fanya mambo yako.
 
Bro ukikutwa na Mali ya wizi, ni kosa, uwe umeokota, au kununua, ilibidi uiwasilishe polisi baada ya kuiokota.
 
Faida za kitonga ndiyo hizo - komaa ukizubaa unakula ndoo.
 
Ila sio simu..
 
Ukizima hiyo simu na kuitupa wana track laini yako, ukivunja laini na kuitupa wana track namba ulizokua unawasiliana nazo akikamatwa mama yako ataonyesha tu ulipo yani wana wewe hadi useme.

Ukute bahati mbaya alieibiwa aliuwawa wakati anaibiwa hapo ndo unaenda kuunganishwa na kesi ya mauji hata kama utaachiwa utakua umekaa mahabusu siyo chini ya miaka miwili au zaidi maana kesi haina dhamana
 
Wewe ndio mtu wa kwanza nimesikia ameokota simu.
Kuna mtu wangu wa karibu kuna siku alishawahi kuokota simu,alipoiokota akanipigia kunijulisha nikamuambia aitupe fasta,maana nishaona kuna jamaa kibamba huko aliuziwa simu baada ya kuitumia miaka 2 siku hiyo wazee wa obey wakamnyakua kama mwewe,simu ya laki na nusu ilimtoka milioni na kadhaa
 
Kwanza hyo simu ilipookotwa haikuwa na laini?? Kama ilikuwa na laini wewe automatically na huyo bi mkubwa ni wezi

Kama simu haikuwa na laini tena smartphone hyo pia ingekuwa ni moja ya jambo la kustua na kuachana nayo simu nzima inakuwaje haina laini

Wadau sasa hvi polisi wanafanya uchunguzi wa mambo mengi vipi ikategeshwa simu mtaani ya either mmoja kati ya watu waliopotea kama kina soka ukaiokota wewe alafu ukatumika kama kichaka cha kuanzia uchunguzi??? Tuwe makini unaokotaje simu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…