Polisi wameshindwa kumkamata huyu tapeli anayewapiga Walimu kila siku?

Kweli. Walimu ni viumbe wa ajabu sana.
 
Taarifa zote za kiutumishi zinaanzia kwenye kituo chako cha kazi. Boss wako ama Mkuu wako wa kazi ama HR atakwambia kama kuna taarifa yoyote ya kiutumishi inakuhusu wewe ama watumishi husika kwenye kituo cha kazi A au B. Sasa inawezekana vipi wewe mtumishi unapigiwa tu simu na mtu humjui kiutumishi then unafata anachokueleza?! Sawa umemsikiliza, kwanini usiwasiliane na HR, Boss ama msimamizi wako wa kazi kuhakiki ulichoambiwa?! Kuna muda ndo maana Elimu zetu zinadharaulika sana aseeh, sasa mtumishi aliesoma adi Chuo Kikuu anakua hivi je layman wa kawaida tu ama mkulima alieko huko kijijini Mpitimbi si atatapeliwa nyumba ama hata yeye mwenyewe [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Unavyoongelea utapeli basi usihusishe TISS. TISS inajukumu moja kubwa sana kuliko chochote, kukusanya intelijensia kwa ajili na kulinda usalama wa taifa, na majukumu mengine mengi ya muhimu. Hawajamkamata huyo tapeli sababu hiyo kesi haiwahusu.

Utapeli ni petty crime maana yake sio jukumu la TISS, bali polisi. Sasa unachotakiwa kufanya ni uchukue hizo namba na ukashitaki polisi. TISS huwezi kuwaona popote na wala hawajulikani.

Usithubutu kabisa kufananisha uzito wa petty crime na kulinda usalama wa taifa au utakuwa unachafua vitu usivyovijua.
Jifunze tofauti ya vyombo vya usalama na kazi zake, sababu kamwe haziwezi kuingiliana hata iweje.
 
Ukiona polisi hawamkamati mhalifu anayejulikana basi fahamu polisi ni TRA wa
 
Hujanielewa vizuri mkuu. Nimesema huyo tapeli amekuwa akiwatapeli watu kwa muda mrefu bila kukamatwa. Huenda polisi wamemshindwa. Je, ikiwa polisi wameshindwa kwanini TISS wasiingilie kati? Wewe usalama wa nchi na raia unauchukulia kwa uzito gani? Unataka wananchi watapeliwe hadi lini ndipo hatua zichuliwe?

Wewe unaona hii ni petty crime lakini ni crime kubwa kuliko unavyodhani. Unajua huyu tapeli ameishatakatisha pesa ngapi kutoka kwa raia so far? Utakatishaji wa pesa anaufanya huyu jamaa unahatarisha usalama wa taifa. Wewe hutaki TISS waingilie kati una agenda gani na huyu tapeli sugu? Jitafakari kwanza mkuu.
 
Naamini wewe ni TISS mkuu niamini kwamba ninachoamini kuhusu wewe ni sahihi.
 
Unajuaje polisi wamemshindwa kama taarifa yenyewe umeileta leo humu saa 11:08? Umechukua hatua gani juu ya hizo namba? Una uhakika gani kwamba labda polisi hawana taarifa za huyo tapeli kama hata wewe umeshindwa kuchukua hatua yoyote ile ikiwemo kutoa taarifa kwa hao polisi? Una uhakika gani hao waliotapeliwa hawakuwa kama wewe?

Usalama wa raia ni wa ndani na usalama wa mmoja mmoja sababu huyo tapeli hawezi dhurumu watu hata 5000 kwa wakati mmoja acha raia million 60,000,000. Na ukilinganisha huyo tapeli ahatarishi maisha ya watu kwa kifo. Hivyo hiyo hatari yake haikizi hata vigezo vya jambazi wala hata mwizi mkabaji.
Na usalama wa taifa asilimia kubwa ni nje na ni mzito zaidi sababu unahusidha raia wengi kwa maelfu, malaki na mamilion au wote kwa pamoja nchi nzima na matokeo ni vifo vya kikatili visivyohesabika. Na pia unahusisha usalama wa serikali na Rais wake kitu ambaco ni muhimu zaidi kwa nchi kuitwa mchi.

Explain kivipi utapeli wa pesa unaweza hatarisha usalama wa taifa? Hivi unatambua ni kiasi gani mafisadi wanaiba pesa serikalini? Au unamaanisha kitu usichokijua sio hatari?

Sio sitaki TISS waingilie, bali kama nilivyosema; majukumu ya vyombo kamwe hayawezi kuingiliana, na kama ikitokea basi ina maana chombo kimoja lazima kiwe labeled incompetent means kitakuwa ni useless na hakuna umuhimu wa hiko chombo kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…