Polisi Wamkamata Mwanachama wa CHADEMA kwa kosa la kuiba michango ya Tundu Lissu

Polisi Wamkamata Mwanachama wa CHADEMA kwa kosa la kuiba michango ya Tundu Lissu

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Fredrick Mbwambo, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa tuhuma za wizi wa fedha za michango zilizokuwa zikikusanywa kwa ajili ya Mwenyekiti wa chama hicho aliyeko gerezani kwa tuhuma za uhaini, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Januari 28, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo, mtuhumiwa huyo alikamatwa jana tarehe 27.01.2026 kufuatia malalamiko rasmi yaliyowasilishwa na Alute Mughwai baada ya kubainika kutokea kwa wizi wa fedha hizo.

“Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za kampuni tofauti za simu na inadaiwa zilihamishiwa kwenye namba mbili za simu moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ni kampuni ya simu ya nchi jirani”, imeeleza taarifa hiyo.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa jalada la shauri hilo limekwishafunguliwa na uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini kiasi halisi cha fedha kilichoibiwa.

Aidha, Polisi mkoani Arusha wamesisitiza kuwa jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushirikiana na Mbwambo katika mtandao huo wa wizi zinaendelea, pamoja na kutafuta vielelezo kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Mbona una comment irrelevant acha kuonesha ujuha wako majukwani humu mshana Jr umekua kilaza sana siku hizi Reviser BlackBold
 
Mi nilionya tangu mwanzo vitendo vya upigaji
20250417_093236.jpg

Na huku ulionya?
 
Kwani Hela zilikuwa zinaingizwa kwenye akaunti ya nani na huyo mwanachama anaitwa nani?
Kwenye Account ya Allute Mugwai Lissu ambaye ndo kaka wa Lissu na ndo mlalamikaji Mwizi anaitwa Fedrick Mbwambo
 
Afadhali umejibu kama mtu mwenye akili timamu. Sasa kama Hela zilikuwa zinaingizwa kwenye akaunti ya Alute,Sasa Fredrick kawezaje kuziiba?
Hapo sasa ndo linakuja suala ya wizi kachota fedha bila ridha ya Allute Kuna kitu kinaitwa Cyber Crime hujawahi kusikia hivyo vitu?? Hujawahi kusikia watu wanaibiwa pesa hata kwenye account za benki ukiacha mitandao ya Simu? You are living on your own planet 😁😁😁
 
Back
Top Bottom