Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Mimi siyo mwanasheria lakini hii inawezekana ni 'maagizo toka juu'. Kwa nini maagizo hayo yatolewe? Ni lazi TAL anyamazishwe at any cost including kubambikia. Anaweza kuchomwa sindano yenye madawa halafu akapimwe. Anaweza akawekwa mahali ambapo anaweza kupewa kilevi fulani (labda bila hata yeye kujua) akipimwa inakutwa cocaine.

Sidhani kama tanzania imefika katika hali hii ingawaje ni rahisi kuamini kuwa huko ndo tunakoelekea. Wanasheria watakwambia kuwa scooe uchunguzi ni prerogative ya DIC. Sasa hiyo ina uhusiano gani na uchochezi, hebu wanasheria watudadavulie.

Kwa maoni yangu udikteta sasa umekomaa!
 
Nizamu ya kumwonesha Nini maana ya Serikali
na ajue
Tanzania nimuhimu kuliko Lissu
 
Mkojo unahusiana vipi na uchochezi? Hii nchi ngumu sana kwakweli
Big brother, kuna tatizo gani kupwimwa mkojo kubaini kama mtukanaji hakupovushwa na ngada?
Tusiwe wasahaulifu kila dakika iendayo kwa Mungu. Juzijuzi tu hapa Manji alimtukana Makonda. Kuja kumpima kumbe ngada ndiyo ilimpa jeuri.
Na isisomeke kupima ni kubambikia mtu, hapana.
Mbn bishop Gwajima alipimwa akaonekana fit?
Acha asorozwe kojo lake huyo mheshimiwa tuone kama kweli jaziba aliyopandisha siku ile, ilikuwa "natural"?
 
Probably Lissu anachochea akiwa under influence/intoxicated. Lissu lazima apimwe kama anatumia sembe.
Sembe haina uhusiano na huo Udikteta bali wanasaka mbinu za kuwakomoa tu lakini wakumbuke malipo ni hapa hapa Duniani walikuwepo akina Chiluba jirani hapo Leo hii wapo wapi?
 
Lissu ana mawakili. Nashauri akubali kutoa mkojo (hata damu) lakini uwe kwenye sehemu mbili:

- moja inakwenda kwa mkemia mkuu wa serikali na ya

- pili iende kwenye independent lab ya upande wa utetezi ikisimamiwa na mawakili wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sembe haina uhusiano na huo Udikteta bali wanasaka mbinu za kuwakomoa tu lakini wakumbuke malipo ni hapa hapa Duniani walikuwepo akina Chiluba jirani hapo Leo hii wapo wapi?
Kwani kipimo ni hukumu?
 
Kinachoendelea hapa ni mambo mawili
1. ''Kumdhalilisha'' kwa kumpelekea kwa mkemia ionekane anatumia vitu vibaya
2. Kumpekua nyumbani, kumpitisha kwa mkemia ni kuvuta muda, leo ni Ijumaa ili alale mahabusu hadi J3

Bila kuingilia suala lililompeleka Polisi, kuna matumizi mabaya ya nguvu na mamlaka
Haya yanajenga chuki katika jamii.

Kesho utashangaa watu wanajiuliza kwanini kuna chuki ya wananchi na taasisi za umma kama Polisi.
Hivi haya ynapokelewaje na wananchi?

Sheria ifuatwe ili ifuate mkondo wake.
 
Back
Top Bottom