Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'

Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Baada ya kuwepo kwa video zinazosambaa mtandaoni kuhusu mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni Afisa wa Usalama wa Taifa mwenye jina la Derick Junior kumpiga raia kwa kitako cha bunduki wakati akiwa kwenye 1234 club huko Masaki, Jeshi la Polisi hatimaye limetoa tamko.

Kwenye tamko lao, Jeshi La Polisi limethibitisha kumkamata mwanaume huyo na kusema kuwa kwa sasa wako kwenye mchakato wa kumpeleka kwenye hatua nyingine za kisheria.

Aidha Jeshi la Polisi lilisisitiza kuwa litamchukua hatua kali mtu yeyote anayemiliki silaha na kuitumia isivyopaswa.

Soma pia: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

IMG_20241028_122321_752.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Derick Derick Junior (36), mkazi wa Salasala, Kinondoni ambaye picha mjongeo (video) zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii akitishia watu kwa silaha.

Taarifa iliyotolewa na Polisi imesema uchunguzi umebaini tukio hilo lilitokea Oktoba 10, mwaka huu saa 12:30 asubuhi maeneo ya Masaki ‘1245 night club’ Kinondoni ambapo mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru sehemu ya jicho na pua kwa kumpiga na kitako cha bastola.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika vyombo vingine vya sheria haraka iwezekanavyo,” imeeleza taarifa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayemiliki silaha, atakayebainika kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizoainishwa katika kibali chake cha kumiliki silaha.

Source: Swahili Times, X Page.
 
Wakuu,

Baada ya kuwepo kwa video zinazosambaa mtandaoni kuhusu mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni Afisa wa Usalama wa Taifa mwenye jina la Derick Junior kumpiga raia kwa kitako cha bunduki wakati akiwa kwenye 1234 club huko Masaki, Jeshi la Polisi hatimaye limetoa tamko.

Kwenye tamko lao, Jeshi La Polisi limethibitisha kumkamata mwanaume huyo na kusema kuwa kwa sasa wako kwenye mchakato wa kumpeleka kwenye hatua nyingine za kisheria.

Aidha Jeshi la Polisi lilisisitiza kuwa litamchukua hatua kali mtu yeyote anayemiliki silaha na kuitumia isivyopaswa.

Soma pia: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Jamaa linagombania utelezi na ukute ni mchepuo fala kweli afu et ni usalama💩💩
 
Back
Top Bottom