Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'

Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'

wanawake wenyewe wa mikorogo hawa, kah! ndio nigombane na mwanaume mwenzangu nilishaikataa hii
Ni hivi, hawa vijana kinachowakuta ni laana, huwa wanatumika kuua na kuteka watu, sasa zile Dua za ndugu wa Marehemu (KURJUAN) ndio zinasababisha anakamatwa kibwege kwa kugombania demu mchafu.

Wengi wao ukiacha kujua kuteka na kuua ni Washamba sana wa mambo mengi mno!

unagombea demu club wakati midemu imejaa kila kona!
 
Wakuu,


Baada ya kuwepo kwa video zinazosambaa mtandaoni kuhusu mwanaume mmoja aliyedaiwa kuwa ni Afisa wa Usalama wa Taifa mwenye jina la Derick Junior kumpiga raia kwa kitako cha bunduki wakati akiwa kwenye 1234 club huko Masaki, Jeshi la Polisi hatimaye limetoa tamko.

Kwenye tamko lao, Jeshi La Polisi limethibitisha kumkamata mwanaume huyo na kusema kuwa kwa sasa wako kwenye mchakato wa kumpeleka kwenye hatua nyingine za kisheria.

Aidha Jeshi la Polisi lilisisitiza kuwa litamchukua hatua kali mtu yeyote anayemiliki silaha na kuitumia isivyopaswa.

Soma pia: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Porojo tu hz, huyo hafanywi kitu, kwanza inawwzekana hata sasa hv ameishapewa likizo, yupo Nairobi, kama tukio la afande na binti kubakwa, Yule afande hajafanywa kitu, hapo hakuna kitu, the goose is already cooked
 
wanawake wenyewe wa mikorogo hawa, kah! ndio nigombane na mwanaume mwenzangu nilishaikataa hii
Derick unagombea mwanamke wa kilabuni kwa bastola.umemkuta kilabuni.yaani unataka kumuua mwenzio kwaajili ya mwanamke wa kilabuni? Ukizubaa SHETANI huwa anaondoka na fikra zote.saa hizi ndiyo amemrudishia Derick fikra zake
 
Back
Top Bottom