PreGE2025 Polisi wasema wamemkamata Golugwa kutokana na taarifa za siri kuwa anasafiri bila kufuata sheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyo "KAIMU" anaitwa nani?
Jumanne Muliro anaumwa au yupo likizo?
Atachukuaje likizo wakati muhimu kama huu? Jeshi la Mama Samia linamhitaji kila askari aliyepo sasa hivi kwenye mapambano haya.
 
Hujui wewe huyo Golugwa aweza kuwa sio raia ana uraia wa nchi mbili na passport za nchi mbili za majina tofauti

Akitoka nchini anasafiri na passport ya nchi nyingine sio ya Tanzania kwa sababu za kigaidi
Bange unayovuta mkuu nadhani sio ya nchi hii
 
Kosa kubwa sana hilo
 
Fezea ndio nini? 😁😁
 
Nimeelewa wanachofanya hawa jamaa. Ni kwamba jamaa atakuwa alikuwa kwenye orodha ya watu wa kukamatwa, sasa wanamsubiri aingie mazima ndo wamkamate wampe aina ya kesi wanayotaka
 
We danga kapeleke genye zako huko, we unawapangia jeshi la polisi cha kufanya? Mmebambwa wanaharamu nyie. Mmenunuliwa kuiharibu nchi yetu kamwe hamtaweza.
 
utaratatibu gani ni mfanyakazi wa serikali?. Hii kweli CCM hakuna akili na idara zenu.

Kuna mda unajiuliza VIZA yangu Passport yangu,Tiketi yangu alafu umri sio wakupangiwa Hivi nyie jeshi mnaongozwa na muriro akili upepo wa kisulisuli hii kauli
We bwege huna unalojua
 
Ukimuona sehemu mtoto anafanya mambo yake ya kitoto mfano kuchezea udongo, nk. Nadhani huwezi kushangaa! Ila ukipita sehemu ukamkuta mtu mzima, halafu anafanya mambo ya kitoto! Nadhani utajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
 
Yaani "anaondoka na kurudi nchini bila ya kufuata taratibu za kisheria"! Ndiyo taratibu zipi hizo kwa wenzetu mnaosafiri kwenda nje?

Ana kesi mahakamani inayomzuia kusafiri bila ya kibali cha mahakama!!

Anasafiri bila ya hati ya kusafiria! Au anasafiri na kurudi kwa kutumia ungo! Na inakuwaje aruhusiwe kupita kwenye mifumo ya ulinzi iliyopo kwenye uwanja wa ndege?

Wataalamu wa sheria, msaada wenu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…