Polisi wasema wivu wa mapenzi chanzo mauaji ya watu 7 wa familia moja Kigoma

Polisi wasema wivu wa mapenzi chanzo mauaji ya watu 7 wa familia moja Kigoma

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya watu sita (baadaye alifariki Mtoto hivyo idadi ya vifo kufika7) bwana Peter Morris (33) wakati upepelezi ukiendelea.

Taarifa za awali zinadai Peter Morris alikuwa akimtuhumu January Mussa (marehemu) kutembea na mke wake.

=====================

Akiri kuua watu saba Kigoma kisa wivu wa mapenzi
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha kumkamata mkazi wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji Peter Moris ambaye ni fundi ujenzi akituhumiwa kwa mauaji ya watu saba wa familia moja katika kijiji cha Kiganza mkoani Kigoma yaliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkuu wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamishna Liberatus Sabas amesema mtuhukiwa Peter Moris amekamatwa Mjini Kigoma na wamejiridhisha kuwa mtuhumiwa ametekeleza mauaji hayo peke yake kwa kutumia panga na kwamba baada ya kumhoji amedai sababu ni marehemu January Mussa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake.

Aidha Kamishna Sabas amesema wananchi wametoa ushirikiano mkubwa kufanikisha kukamatwa kwake na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ambapo pia ameeleza kuwa idadi ya waliokufa imeongezeka baada ya mtoto aliyejeruhiwa kufariki mkoani Morogoro wakati akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya taifa ya muhimbili.

Kwa upande wake Mratibu wa kanda ya magharibi wa mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania THRDC Alex Luoga amelaani tukio hilo na kuitaka jamii kutumia njia sahihi na za kisheria kumaliza matatizo.
 
Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya watu sita (baadaye alifariki Mtoto hivyo idadi ya vifo kufika7) bwana Peter Morris (33) wakati upepelezi ukiendelea.
Taarifa za awali zinadai Peter Morris alikuwa akimtuhumu January Mussa (marehemu) kutembea na mke wake.
Mkuu unaonaje ukae utulie baadae uje na habari kamili
 
Kuna mmoja alilieta mazoea nikapiga nikasepa. Nikamchunia mpk leo na sijawahi kumtafuta huu ni mwaka sasa. Sitaki mazoea na wake za watu kabisa. Hawa kukua ni dakika 1 tu ushakufa.

Wake za watu siyo poa ila kutoa mbususu huwa hawajivungi na hubaniwi. Mkihaidiana muda wa kupiga show, ni show siyo wale umpe nauli , umnunulie chips na umwagie nje
 
Hizi taarifa za awali siziamini,kama ni polisi ndio wanasema hivi kuna walakini hapa,wameshindwa kufanya kazi wanakuja na taarifa za awali ili baadae ndio iwe imetoka hio.

Mtu unahisi anatembea na mkeo ndio uue familia nzima hadi watoto wadogo?halafu haohao polisi walisema waliofanya mauaji hayo sio mtu mmja,kuna shida hapa
 
Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya watu sita (baadaye alifariki Mtoto hivyo idadi ya vifo kufika7) bwana Peter Morris (33) wakati upepelezi ukiendelea...
Hivi kwanini ule mali ya mtu tena iliyotolewa mali pia? Uku kwetu anakufa mhusika pekee afu fresh tu wazee wa kijiji wanahalalisha tukio.
 
Back
Top Bottom