Polisi watia fora maandamano CHADEMA: Polisi wanaanza kuelewa kuwa upinzani siyo uadui!

uadui ni maneno ya kichochezi na ubishi wa viongozi wa kisiasa 🐒
 
"Ukikua" utaelewa
Hapana mkuu. Yaani hapa nilipo ni mtu mzima naweza hata nikawa baba yako lakini sijawahi kuelewa haya mambo ,sijui lakini labda mie ni mjinga.

Mie naona Hii ni kama mentality fulani ambayo tunarithishwa inakua kama chain babu, baba, mtoto. Asee mie niligoma kurithi haya mambo mzee. Mpira na siasa. Yaani hata katika maisha ya kawaida nikikuona una hisia kali sana kuhusu siasa huwa naona hata katika mambo mengine ya kila siku kuna shida.

Kuna siku nilikua bar. Kukawa na mechi kati ya yanga na tp mazembe nadhani, yanga alishinda kula jamaa mmoja mtu wa makamo tu nikamuona kasimama analia huku anasema "asante yeesu!! Asante yesuuu! Asante yesuuu" kwa akili ya kawaida unaweza kuchukulia poa, ila ukitazama kiundani unaona kabisa huyu mtu kuna sehemu atakua na shida fulani, yaani mtu mzima wa makamo (45_55) goli limefungwa unalia mhhh?
 
Safi mnawaongezea CCM pesa kwa ajili ya kuendelea kutawala!
 
Ukiona hivyo jua kua upunzani sasa hauna maana tena... hauna impact..
 
Tumetokaa Mbaliii Tumemfataa...
 
Samahani lakini una umri gani?
 
Samahani lakini una umri gani?
Usitazame saana suala la umri wangu mkuu coz naweza hata nikawa baba yako(ki umri), ila tujaribu kutumia Common sense hebu jaribu kuzama deep kimawazo. Usisikilize makelele ya tv sijui redio wala makelele ya wanasiasa(vyama vyoote kutia ndani ccm) jaribu kuji factory reset halafu uyatazame hayo mambo ukiwa nje yake. Ukiangalia sana utaona ni maujinga fulani tu. Usikubali kuendeshwa na hisia
 
Hayo ni matembezi tu kama matembezi ya meimosi
Maandamano ya kweli yenye kuleta mabadiliko ni yale ambayo polisi wapo upande ule na bunduki mabomu ya machozi na magari ya washawasha na raia tupo upande huu
Hayo ndiyo maandamano yaliyo fanyika Kenya, Tunisia, Iran, Ufaransa, Marekani

Na siyo hayo maigizo ya walamba asali.
 

Sio polisi, ni CHADEMA wameanza kuelewa kumbe kuandamana sio kuharibu mali na kuiba mali za watu au kuleta vurugu, Chadema walikuwa wajinga sana wakiandamana wanaharibu mali za watu na kuiba na kuleta vurugu kubwa, CHADEMA ndio wamameanza kupata uelewa kidogo, kama unakumbuka mlikuwa mnasemwa mna akili za nyumbu, yaani maana yake akili za Chadema ilikuwa kama za nyumbu..

So si polisi, ni Chadema unyumbu umeanza kuwatoka taratibu mnaanza kuwa na akili za kibinadamu..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…