Polisi wavamia CHADEMA Karatu ni muendelezo wa siasa zilizopitwa na wakati

Polisi wavamia CHADEMA Karatu ni muendelezo wa siasa zilizopitwa na wakati

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
FB_IMG_1620426189724.jpg
 
Wamevamiwa na Tanpol

Tanpol ndio nini ????

Fomu za wagombea wetu zilikuwa zinachanwa na Tume ya Uchaguzi. You can now see part of the reason why. Sehemu za kujaza jina la chama tulikuwa tunaandika MOVEMENT FOR CHANGE!

Hatujifunzi.
 
Tuweke masihara pembeni, toka John arudishe usajili kwa Sir God vyama vya upinzani na wafanyabiashara wamepata likizo ya mapumziko kwa miezi miwili sasa.

Yule mzee alikua katili, ilikua hazipiti siku mbili bila mwanachama wa upinzani kung'olewa meno, kuswekwa ndani, kuvamiwa na kutekwa. Wafanyabiashara nao hazipiti siku tatu kuchezea kesi za uhujumu uchumi na kukwepa kodi.

Ilikua ndani ya siku 5 taifa linapokea mpaka Breaking News 400, hujui uanze kusoma breaking news ipi na uache ipi. Roho zilikua juu juu kila dakika. Hata uamke saa 8 usiku unakutana na breaking news.

Mungu asante kwa hilo. Taifa limepumua.
 
Nadhani sasa mama anatakiwa atoe japo kauli ya kiuongozi ili hao wafahamu sasa ni awamu nyingine!!kwa sasa siasa zile za kishamba hazina nafasi!!kwani anavyo yakalia kimya tu, sio picha nzuri, wakati wananchi wana imani naye kuonyesha mwanga mpya!!
Kwani wewe ni akili ya mama kama unataka u raisi si ugombee yaani kila kitu mama polisi wafanye yao eti mama sema Acheni majungu
 
Eti mama! Kwani amekuzaa acheni kujipendekeza
 
Rudi CCM ,nakuona siku hizi umekuwa msemaji Wa CCM ,nyie kwa akili zenu za kuambiwa itawachukua miaka 1000 kuitoa CCM madarakani

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Rais mara nyingi anazungumzia kukuza uchumi tu, mambo ya demokrasia bado yupo kimya sijui anasubiri nini, au ndio ule muendelezo wa kauli yake aliyoitoa Mbeya kwenye kampeni za CCM hata wasipoichagua CCM ndio itakayounda serikali.

Hicho kichwa cha habari ningependa kibadilishwe, sio fair kumtupia lawama asiekuwepo, tukiendeleza hii tabia haya matendo ya kionevu kwa wapinzani yataendelea kwasababu mnashindwa kumkemea mtu sahihi.
 
Kiukweli tumepumua,vifo, stress vimepungua, natumai hata uhitaji dawa kuweka BP na sukari sawa umepungua,Asante Mungu Baba kwa muujiza na zawadi ya Mama.Hili la Karatu asubuhi mapema watajirudi, tunashida na majambazi na vibaka sio democrasia.
 
Tuweke masihara pembeni, toka John arudishe usajili kwa Sir God vyama vya upinzani na wafanyabiashara wamepata likizo ya mapumziko kwa miezi miwili sasa.

Yule mzee alikua katili, ilikua hazipiti siku mbili bila mwanachama wa upinzani kung'olewa meno, kuswekwa ndani, kuvamiwa. Wafanyabiashara nao hazipiti siku tatu kuchezea kesi za uhujumu uchumi na kukwepa kodi.

Ilikua ndani ya siku 5 taifa linapokea mpaka Breaking News 400, hujui uanze kusoma breaking news ipi na uache ipi. Roho zilikua juu juu kila dakika. Hata uamke saa 8 usiku unakutana na breaking news.

Mungu asante kwa hilo. Taifa limepumua.
Sasa taifa linapumua vipi kama bado wapinzani wanakataliwa kufanya hata mikutano ya ndani? haki inakandamizwa unashangilia kisa mkandamizaji sio mwendazake!

Uminywaji wa demokrasia upo wa aina nyingi sio lazima kuteka na kupiga wapinzani, hata kuwanyima kufanya shughuli zao za kisiasa kinyume cha sheria ni ukatili pia lazima ukomeshwe, sioni nafuu hapo.
 
Upo sahihi mkuu,sasa hivi chadema wapo kuisifia ccm huku wakisahau kupigania mambo yao ya msingi
 
Hili liko wazi! Huyu mama anaongea kisiasa tu hamna jipya.. sema watz ni wasahaurifu sana.. nikuwaacha kwanza watakuja kujionea mbele ya safari.
 
Nyie Chadema hebu andikeni list yenu yote mnayotaka mama afanye muiweke hapa tuijadili maana kila kitu nyie mnataka mama afanye mtakavyo.Kila mtu amekuwa mshauri wa mama.Kila jukwaa mnamshauri mama hata MMU mnamshauri awe na mume aina gani.
 
Back
Top Bottom