Tuweke masihara pembeni, toka John arudishe usajili kwa Sir God vyama vya upinzani na wafanyabiashara wamepata likizo ya mapumziko kwa miezi miwili sasa.
Yule mzee alikua katili, ilikua hazipiti siku mbili bila mwanachama wa upinzani kung'olewa meno, kuswekwa ndani, kuvamiwa na kutekwa. Wafanyabiashara nao hazipiti siku tatu kuchezea kesi za uhujumu uchumi na kukwepa kodi.
Ilikua ndani ya siku 5 taifa linapokea mpaka Breaking News 400, hujui uanze kusoma breaking news ipi na uache ipi. Roho zilikua juu juu kila dakika. Hata uamke saa 8 usiku unakutana na breaking news.
Mungu asante kwa hilo. Taifa limepumua.