Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Jeshi letu linaongozwa na watu wenye upeo mdogo sana. Kwa kupanga hii mbinu chafu yenye lengo la kufanya kitendo kilicho kinyume cha katiba, kwa upeo wao mdogo walio nao, wanaona wametumia mbinu ya akili kubwa sana, kwa sababu ndipo upeo wao unapoishia.Polisi Tanzania wametoa taarifa kuwa maandamano yaliyopangwa kufanyika na uvccm nchi mzima hayataruhusiwa
Wametoa sababu Kuwa kufanya hivi kunaweza kusababisha taaruki kwenye jamii
View attachment 2690293
My take,
Hii Ni mbinu zilizopangwa kati ya uvccm na vyombo ya ulinzi, ili kupata sababu ya kumzuia mwamba MDUDE asiweze kufanya maandamano ya vijana nchi mzima kupinga mkataba wa bandari
Polisi Tanzania inabidi itambue kuwa kuandamana Ni takwa la kisheria ,na si utashi wowote wa mtu au taasisi kuamua lini na Nani aandamane ikiwa maandamano ni ya amani
Mdude chadema anataka kufanya maandamano ya amani, kwa kile anachoona kuwa rasilimali ya nchi inataka kupotea kiraisi, naomba jeshi letu la polisi liheshimu nia yake
Wakumbuke kuwa kutetea rasilimali ya nchi ipo kwa mujibu wa sheria
Polisi na huyo mwenyekiti wa UVCCM, watambue kuwa wananchi wana akili zaidi yao maradufu, vimbinu vya kijinga kama hivyo havina msaada wowote.