PreGE2025 Polisi yatoa onyo kali, yasema haitavumilia vurugu uchaguzi mkuu Oktoba

PreGE2025 Polisi yatoa onyo kali, yasema haitavumilia vurugu uchaguzi mkuu Oktoba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
tutakula sahani moja na wahuni wote awamu hii wallah

mwananchi usikubali kutumika kuichafua amani ya nchi hii na kikundi cha kisiasa cha no sijui kitu gani
 
Sisi hatutashiriki labda mpigane nyie wenyewe wakuu mana mmesema mpo 13 Million hivyo mnatosha kabisa mkiibiana kura
Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kuelekea na wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, likisema halitakuwa na muhali katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, utulivu na usalama wa hali ya juu.

Kauli hiyo imetolewa Ijumaa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji, wakati wa sherehe ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Mdogo wa Jeshini ngazi ya Sajini (kozi namba 2-2024/2025), yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi.

Awali, Kamandanti wa Shule ya Polisi Tanzania, SACP Ramadhani Mungi, alitoa taarifa kuhusu mafunzo hayo, akibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 2,078 walijiunga na mafunzo hayo Machi 14, 2025, kutoka mikoa na vikosi vyote nchini. Kati yao, wanaume walikuwa 1,704 na wanawake 374.

Katika ripoti yake, SACP Mungi alisema kuwa wanafunzi 2,068 ndio walihitimu rasmi, huku wanafunzi tisa wakiachishwa mafunzo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo utovu wa nidhamu, na mwanafunzi mmoja alifariki dunia kwa ajali ya gari.

Kwa mujibu wa Kamishna Awadhi, wahitimu hao watatumika katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhakikisha kuwa wakati wote wa kampeni, upigaji kura na baada ya uchaguzi, hali ya usalama inabaki kuwa shwari na vyombo vya dola vinaendelea kuwa katikati ya kuhakikisha haki inatendeka bila upendeleo.

View attachment 3351882
 
Warrior wa mitandaoni una vituko bwege wewe
Wewe unaeleweka nini kinachokupa msukumo hapa JF wa kumtetea Samia na Genge lake.
Ni wajibu wetu waTanzania wapenda haki kukabiliana nanyi mahali popote pale.
Hii ni vita ambayo hamtaruhusiwa kuishinda. Elewa hivyo.
 
Wewe unaeleweka nini kinachokupa msukumo hapa JF wa kumtetea Samia na Genge lake.
Ni wajibu wetu waTanzania wapenda haki kukabiliana nanyi mahali popote pale.
Hii ni vita ambayo hamtaruhusiwa kuishinda. Elewa hivyo.
Welcome to the war
No fear here
 
Back
Top Bottom