Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jeshi la Polisi nchini limewaachilia kwa dhamana viongozi wa CHADEMA waliokamatwa kutokana na tuhuma mbalimbali. Kati ya viongozi hao ni Makamu wa Kiongozi wa CHADEMA, John Heche, Naibu Katibu Mkuu, Aman Golugwa, Kiongozi wa Chama Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu 'Boni Yai' pamoja na mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.

Viongozi hao wameachiliwa leo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, baada ya kukamatwa na kushikiliwa katika vituo tofauti vya polisi kwa nyakati tofauti. Taarifa hiyo imetolewa na CHADEMA wenyewe katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Pia Soma: Polisi: Gwajima, Golugwa, Brenda Rupia, Lema, Mahinyila na Mnyika wajisalimishe katika vituo vya Polisi
1762790124484.png
 
Wakikubali maridhiano watakua wameusaliti umma wa watanzania kwa kiasi kikubwa sana. Watanzania waliokufa ni wengi sana
Wakiridhiana na wahuni ni heri yao wenyewe. Siye umma hatuko nao. Wananchi tuko peke yetu, hatuna uhusiano na wala hatuwakirishwi na chama chochote. Hatuna msemaji. Sisi ni sisi. Waridhianie wasiridhiane sisi mambo yetu yako pale pale….

Sisi hatuwahitaji Chadema, lakini Chadema bila sisi si kitu chochote. Wajitafakali.
 
Wakiridhiana na wahuni ni heri yao wenyewe. Siye umma hatuko nao. Wananchi tuko peke yetu, hatuna uhusiano na wala hatuwakirishwi na chama chochote. Hatuna msemaji. Sisi ni sisi. Waridhianie wasiridhiane sisi mambo yetu yako pale pale….
Naunga mkono hoja!!!..na wakijaribu kurilidhiana wao ndio watakaolipa damu za vijana wetu .tutaenda nao kiulaloulalo
 
Back
Top Bottom