POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

Umeongea ukweli bro..wengi ambao tupo addicted na alcohol tunakua very depressed and tunakosa perfect person wakuwaelezea what we are passing through...so it's kill slowly
nafurahi kukutana na watu wanaojua ukubwa wa tatizo hili na ukweli utabaki palepale. Walevi ni wapenda sifa na hata wakiwa na maumivu sio rahisi kuwajua maana hupenda kuonekana wako vizuri
 
Sijakataa watu wa design yako kama wapo? Ila elewa na wa design hii wapo pia tena wengi. Huwa tuna hesabu na maamuzi mazuri kabla ya kulewa lakini tukishakuwa tumelewa maamuzi hayo huyeyuka. Unaweza usikope lakini ukatumia zaidi ya ulichokuwa umepanga yote ni ufujaji wa pesa
 
Nilipokuwa mlevi nilipokutana na watu wanaoiponda pombe nilikuwa nawaona kama wachawi na nilikuwa naitetea kwa namna yeyote ile ili ionekane hakuna shida kulewa lakini kwa sasa huwezi kunidanganya ndugu hayo maneno ya shombo hata mimi nilishaambia sana watu. Tuache tu sababu hatujuani lakini kwenye pombe sikuwa boya kama unavyodhani
 
Kama ni Mdau Kikosi cha kwanza ukiingia Picnic unaanza kugombaniwa na mademu kabla hujakaa 80000 imeshakatika....

300000 unaweza KUSTABULAIZI mikikimikiki

Arusha Dolali zinatupa KIBULI
 
Si muda mrefu sana ni miezi mitano tu sasa tangu niache naimani sitarudi tena
Maamuzi mazuri sana kila la heri ufanikishe ila pombe ni jini na binadamu wa kawaida kushindana na nguvu za giza yahitaji commitment ya hali ya juu na kumshirikisha mungu.

Mwanamke anayeweza kuishi na mlevi huyo ni super woman BabaMorgan ningekuwa nina uwezo ningeandaa kongamano la kuwapongeza wanawake wanaoishi na walevi na kuwapa zawadi.
 
Nashukuru sana mkuu, kweli wanawake wanaoishi na walevi wanavumilia mengi sana hata wale wanaojiita walevi wastaarabu nao ni shida tupu nimekaa nao mimi unaweza kumuona mstaarabu sana kumbe kuna mambo ya kishenzi anayafanya gizani
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Alafu kuna mtu anashangaa kusikia umemaliza 300k kwenye pombe.
Ninatumia ila point ya jamaa ya kushindwa kuhimili ki akiba inanitesa hadi leo , Nina siku nne za kujitathimini toka Ijumaa sasa sijajua nitafaulu au lah manake nina 15k gheto ngoja nijae visenti nione
 
Mi niliacha pombe baada ya kupiga mzinga wa K Vant mwenyewe tena kavu,asubuhi nilipoamka nikawa naumwa na koromeo siwezi kumeza kitu zaidi ya maji na soda ,week mbili nilikuwa mgonjwa mi mtu wa uji tu . Nilipopona nikasema haya yote ya nini miye? Starehe gani inakuwa mateso ,nilipopona sikuendelea tena nilitumia mwanya huo kuacha pombe kabisa
 
Kama ni Mdau Kikosi cha kwanza ukiingia Picnic unaanza kugombaniwa na mademu kabla hujakaa 80000 imeshakatika....

300000 unaweza KUSTABULAIZI mikikimikiki

Arusha Dolali zinatupa KIBULI

Hahaha msalimie Sophia mhudumu mmoja cheupe hivi na kishundu hatari
 
Mzee hapo ni kupambana kweli kweli kuacha hiyo kitu, uraibu wowote unaumiza, nawajua walevi sababu nimeishia nao, wanangu tulikuwa tunakula bata wote ni walevi mbwa kasoro mimi na huwa namshukuru mungu katika hili, uraibu wangu ulikuwa kwenye kubeti na wanawake, aisee nilikiwa kitoombi, ila wanawake hawakuwa wanaharibu bajeti zangu kama kamari, aisee kamari niliivulia kofia, ila nilifanikiwa kuacha baada ya jaribio la kwanza kufeli.. La pili likatiki, mambo yasiwe mengi nikaoa kabisa, jumlisha kusali sali sasa hivi mwaka wa 3 huu sijacheza kamari, na toka nimeoa mpaka sasa sijapiga mechi za nje(japo hili suala kiukweli najikaza saana, bado napambana[emoji1787][emoji1787]) ila kamari nimeiweza 100%
 
nafurahi sana kukutana na watu wanaojua ukweli wa tatizo hili, kuna walevi uchwara wanajifanya kunishangaa na kujiona wao wameiweza pombe
 
Mbn sijaona pombe apo
 
Sijaona pombe
Huwa sipendi kubishana mambo ya dini lakini ngoja nikueleweshe.
Neno intoxicants kutoka tafsiri ya kiingereza lina maana hii: Any substance that is known to have or does have intoxicating effects, and includes alcohol, marijuana, or any other controlled substances.

Lakini neno hilo kwenye aya hiyo ya Qur'an limetumika kama tafsiri ya neno la kiarabu Khamr ambalo kwa tafsiri rahisi ni kilevi
(wakati mwingine uwe hata una google basi)
 
Unaweza kuweka tafsir ya hiyo Aya hapa?
Maana khamr sio alcohol
 
Unaweza kuweka tafsir ya hiyo Aya hapa?
Maana khamr sio alcohol
Sijasema Khamr maana yake ni pombe bali ni kilevi yani mjumuisho wa vyote vinavyolewesha ikiwemo madawa ya kulevya.

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلْخَمْرُ وَٱلْمَيْسِرُ وَٱلْأَنصَابُ وَٱلْأَزْلَٰمُ رِجْسٌۭ مِّنْ عَمَلِ ٱلشَّيْطَٰنِ فَٱجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

kama utaweza isome yote hapa tafuta mstari namba 90 Kiarabu imeandikwa hivi ٩٠ au seach Google Quran 5:90 in swahili

Surah Al-Maidah ( The Table spread with Food )​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…