Pombe hunywi, sigara huvuti, club huendi; starehe yako ni ipi?

Pombe hunywi, sigara huvuti, club huendi; starehe yako ni ipi?

Situmii pombe,sigara sivuti, club siendi kwasababu nachukia sana kelele hata nikiskia kelele za mtu akigombezwa/kugomba hovyo tu zinanikera naondoka hiyo sehem

Starehe yangu ni mpira ila sibet na timu yangu ni manutd imenitesa kinyama imefika hatua siumii tena hata ikifungwa na mechi siangalii vilevile

Hakuna kinachonipa raha kwa sasa
 
Starehe zangu kubwa

1. Mtoto wa mama mkwe - Hakuna ninachokipenda kuzidi, wakati wetu mimi nae ndio naiona thamani ya maisha.

2. Kupika chakula kizuri watu wale wafurahi

3. Mpira- Team zangu Yanga & Arsenal zikishinda ni burudani tosha.

4. Usafi- Napenda mazingira na kila kitu kiwe safi, napata amani sana.
 
Back
Top Bottom