Pombe ni adui wa mafanikio! Ulevi unapoteza pesa, muda na Fursa

Mkuu sijui nikujibu, sijui niache....?

Kwa ufupi, nina historia mbaya na pombe, niliwahi kulala mahabusu miezi sita ijapo sikuhukumiwa kutokana na tukio nililolifanya...
Imepita miaka 28 sasa sijui kilevi kinaingia vp mdomoni
Sababu ya kukaa nyuma ya nondo haikua bia ila ulikua wewe mwenyewe ndio maana walikuweka wewe nyuma ya nondo wakaacha kuiweka nyuma ya Nondo bia, siku hio ulikunywa bia gani?
 
Sababu ya kukaa nyuma ya nondo haikua bia ila ulikua wewe mwenyewe ndio maana walikuweka wewe nyuma ya nondo wakaacha kuiweka nyuma ya Nondo bia, siku hio ulikunywa bia gani?
Nilikunywa safari (ilikuwa ni miaka 2 tu tokea kuanza kutengenezwa) nikachanganya tusker pamoja na viroba vya no. 1, aisee nikarudi home, nilichokifanya kwa babangu mdogo, alikula kisu, utumbo huo njee, kakimbizwa ddh (hakufa)
Nakumbuka kauli ya mzee hadi leo "WE NGURUWE, MDOGO WANGU AKIFA NA WE UNAFIA JELA"
baada ya miez sita nilivyotoka habusu kwa kweli sitaki mazoea..ijapo nimetembea maeneo meng nje ya bongo, lakn nimekuwa nikijizuia.
 
Pole sana sasa ilikuaje Mzee wako akakuita Nguruwe?
 
Kanuni/sheria tatu za pombe unazopaswa kuzizingatiq muda wore
1 . WEWE NI NANI
2. UKO WAPI
3. UNAFANYA NINI
Ukishasahu zote ama moja kati ya hizo achana na pombe haraka sana
 
Nikifikiria sana kwanini vijana wengi tumeingia kwenye mtego huu, huwa na hitimisha kwa kuamini shetani yupo kazini. Ulevi sio kuwa ni mtindo wa maisha tu, hapana! Ni mkakati wa kuzimu kufanikisha agenda yake ya kuwaongoza watu kwenda kwenye umasikini, magonjwa, zinaa na hatimaye jehanamu.(Ufunuo2:14)
Zinahitajika jitihada za makusudi za kiroho na kimwili kujinasua na kuwanasua wengine kutoka katika kifungo hiki cha giza.
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…