Kama ilikuwa picha ni lazima kuwekwa basi alikosa kazi kihalali kabisa, kwa nini alipuuzia, au kwa sasa amekosa uwezo wa kuona vitu kiumakini, attention to detailsNiliogopa kwa sababu mtu aliyepo serious hawezi kufanya hivyo; Namaanisha uchaguzi wao niliufananisha na kuchagua Shaba kwa sababu ipo kwenye boxi la chuma na kuacha Almas kwa sababu ipo kwenye box la mbao.
Au pengine mgonjwa asijekuchanganyiwa dawa kwa makosa, huku tumeacha ma genius mtaani kwa sababu ambazo kimsingi hazina mashiko...
Nakubaliana na waziri, kipindi niko serikalini uvaaji sahihi ilikuwa muhimu mnoo na kulikuwa na dressing code kabisa.Wangekuja na katai na kashati wote laki mbili wangepata!?
Nadhani maisha yaendelee wamepewa waliopewa waliokosa ni kupambana hadi tufike mwisho
Hao walioenda usaili wako serikalini!?Nakubaliana na waziri, kipindi niko serikalini uvaaji sahihi ilikuwa muhimu mnoo na kulikuwa na dressing code kabisa.
Utumishi wa umma kuna mavazi yakeKuna taaluma binafsi nikimuona mtu kaja na jeans na t-shirt na chini raba tu yakawaida kifupi yuko simple, na nywele amenyoa Tu kawaida yaani nywele fupi NAMPA KAZI HARAKA SANA, Kwa uzeofu wangu hawa huwa niwapiga kazi sana na wako real.
kuna dada aliomba nafasi ya Nursing kwenye Hospitali yetu kubwa na huku ana GPA 4.7 akakosa kwa sababu barua yake ya maombi haikuwa na picha ya passport, pamoja na kwamba vyeti vyake vilikuwa nayo..wakaishia kuchukua mtu wa GPA sijui ya 3.4 aliyeweka picha ya passport kwenye barua ya maombi. Ukweli niliogopa sana...
Huko Serikalini wapo serious sana....
Shati la buku kweli la kulivalia tai?Ha ha ha waziri amesema shati ni buku tai labda ndiyo inabidi ugongee
Huwezi kwenda kwenye usaili umenyoa kiduku, umevaa kata K, umevaa jeans na Tshirt ina picha ya kitu cha Arusha halafu utoboe...niko pamoja na WaziriHao walioenda usaili wako serikalini!?
Wewe ndo unapanic kipumbavu...Hizo picha za hayo mavazi ziko wapi?, Wewe mleta mada umeyaona wapi mavazi hayo? Acha kuleta nada za kipumbavu na wapumbavu wako wa ccm.
Kumbe vyeti na uwezo wa mtu sio muhimu sana....kuvaa na maisha binafsi ya mtu iwe sifa kuu ya mtu kupata ajira na siyo weledi wake.Habarini wakuu
Nimeona hii habari ikieleza sababu za wengi kushindwa Usaili wa ajira mbalimbali zinazotangazwa serikali
Sababu hizo zilizotajwa ni pombe, uvaaji usiofaa na mitindo ya nywele kwa wale wanaoitwa hasa kwa usaili wa mahojiano
Nukuu kutoka kwa Waziri Simbachawene "Mwalimu anakuja amevaa jeans imekatikatika humu eti anakuja kwenye Usaili wa ana kwa ana. Njoo kwenye usaili umepiga katai kako na kashati kako. Mbona siku hizi kwenye masoko kuna hadi ka shati ka 1000 unamwona huyu ana haiba. Wengi wanashindwa kwa namna wanavyokuja"
Chanzo gazeti la Nipashe