Kumbukumbu yangu na marehemu
Siku moja ya Ijumaa mwaka fulani nilifika bar ya River Road kwenye saa tano usiku hivi
By then ndio ilikuwa bar kubwa mitaa yote ya Picha ya ndege na karibia kila weekend ilialika bendi, lakini weekend ile hapakuwa na bendi hivyo muda huo wateja walibaki wale wa kaunta tuu
Nilikuta jamaa wawili watu wazima wameshiba wako counter
Wahudumu waliobaki muda huo walikuwa wawili tuu marehemu na rafiki yake ambaye naye alishafariki hapo hapo Picha ya ndege
Basi nikapewa signal kwamba nisikae counter nikavutiwa kiti pembeni kidogo na kimeza kisha nikapangwa,[emoji3] Kumbe wale jamaa walikuwa Masoja wa Msangani na walishakubaliana na wale mabinti waondoke nao , kumbe wale mabinti licha ya kula na kunywa vya watu lakini hawakuwa tayari
Kutoka River road mpaka barabara kuu ya lami ni kama robo km hivi, hivyo nikapanga na wale mabinti nikikaribia tu kumaliza wao wapite kushoto wakanisubirie mbele. Haya mawasiliano yalikuwa yanafanyika kwa msg muda Wote
Kumbe wale masoja walishastukia mchezo, ile nakaribia kumaliza mabinti wakapita hivi nami baada ya kama dk 3 nikapita hivi nikawasha gari nikaondoks.. Sasa kile kipande kuelekea barabarani kilikuwa na majani marefu almost kama kichaka
Ile nawakaribia kucheki kwenye site mirror naona kuna gari inakuja nyuma yangu, [emoji23] wale mabinti waakazama kichakani kujificha, mimi nikapiga double hazard na kushuka kwenye gari kama nataka kujisaidia,
Jamaa wakaja wakapita pembeni huko wanachungulia kwenye gari. Niliacha mlango wazi kidogo ili waone hakuna mtu mwingine ndani ya gari
Jamaa wakanyoosha mpaka road hola hakuna mtu[emoji23].. Sasa jamaa walipopita mabinti wakachomoka kwenye kichaka na kupanda gari.. Tunafika road tukaona gari yao wamepaki upande wa pili wa barabara kwenye petrol station ya ATN ilikuwa haijaanza kutumika
Dah wakasema hawa jamaa bado wanatufuatilia, na mipango yetu ilikuwa ni kwenda maili moja maana kwa wakati ule ndio palikuwa pamekucha.. Sasa nikinyoosha maili moja jamaa watanistukia mimi nikakunja kuelekea Picha, kuona vile jamaa wakaondoka kuelekea maili moja (kumbe walidhani wale mabinti wamekimbia na boda)
Mpaka nafika Picha ya ndege sioni gari inayonifuata hivyo nikakunja kuelekea njia ya Tumbi nikatokee Maili moja.. Kumbe jamaa wale walikiwasha mpaka TAMCO bila kuona Boda yoyote, hivyo wakastukia janja yangu na kukunja kuingia njia ya Tumbi [emoji23]
Nafika Tumbi napishana na gari yao.. Loh tukastukiana.. Sasa mimi nilikuwa na gari ndogo automatic wao walikuwa na Landcruiser short chassis old model manual... Ile mpaka wao kunistukia na kugeuza nilikuwa nimeshawaacha mbali..
Nitaendelea