Pombe yaua Mhudumu wa Baa aliyekunywa bila kula

Pombe yaua Mhudumu wa Baa aliyekunywa bila kula

R.i.p kwake pole kwa familia haya ni moja ya matukio ya kushtukiza ila naomba tukiwa kama marafiki tukiwa tunakunywa mara nyingine tushauriane kuhusu kula na hata kupata maji ya kutosha, simlaumu yeye lakini pia waliokua nae karibu(kampan) wakati wa kunywa hawajamtendea haki. Mara nyingine watu wanakunywa kutokana na stress kali za maisha hivyo tunavyoonana ama tukiwa tunakunywa tushauriane pia.
 
Hii issue ya 50/50 wanawake wa Kitanzania wanaitendea haki vizuri sana.

Vifo vya kunywa pombe hadi kifo tumekuwa tukiwasikia wanaume ndo wanaokumbwa na hiyo mikasa ila dada zetu wame-advance sasa ni haki sawa "kunywa pombe ufe ninywe pombe nife".
 
Mhudumu wa Baa ya Nyemo, Asia Eliya (24) amefariki dunia kwa madai ya kunywa pombe kupita kiasi bila ya kula chakula.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Picha ya Ndege, Joseph Zambo alisema kuwa Asia alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Zambo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 8, mwaka huu majira ya alfajiri nyuma ya baa kwenye migomba jirani na alipokuwa akifanyia kazi.

"Nilipigiwa simu kuwa kuna mwili wa mtu aliyekufa ilibidi niende na nilipofika niliambiwa mwili umechukuliwa na polisi kupelekwa Tumbi ambapo alikuwa hajafa na alifia njiani," alisema.

Alisema kuwa wafanyakazi wenzake walisema kuwa siku hiyo Asia alikunywa sana pombe kabla ya umauti kumkuta.

"Alichunguzwa lakini hakukutwa na jeraha lolote wala kuumia popote, hali ambayo inaonesha kuwa inawezekana pombe ndiyo ilisababisha kifo hicho," alisema Zambo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alikiri kutokea kwa tukio hilo.

HABARI LEO
Usikute hapo kuna mwamba alikuwa anamtoa offer ili baadae akampige mlingoti ....
 
Iv mtu unakunywa pombe hauli chakula unapata raha gan sasa? Siwezi kunywa bia zaid ya tano bila kutupia nyama choma katikati ,then nalisongesha nne tena napata supu ya kongoro nashushia na maji makubwa , kuna kautamu fulani ka bia unapoisindikiza na nyama choma ,ndiz na kachumbari na pilipil kiasi.
 
Back
Top Bottom