ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Igweeee igweeee!!
Napenda kwanza kukiri kuwa mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba Sc, timu ambayo ni mahasimu wakubwa wa klabu ya Yanga hapa nchini Tanzania.
Bila ya kupoteza muda, napenda niwamwagie salamu za pongezi timu ya Yanga SC, viongozi na mashabiki wake kwa ujumla kwa kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Pongezi nyingi zaidi nazielekeza kwa Kocha Nasrideen Nabi, kwa mara nyingine ameonesha kuwa ni kocha anayelielewa soka la Afrika. Jana amewaduwaza Watunisia wenzake pale Tunis. Mashabiki wa Club Africain hawakutegemea kuiona timu yao ikicheza kama 'underdog' ndani ya ardhi yao ya Tunisia.
Yanga walipiga mpira mkubwa sana, nimekoshwa sana na uchezaji wa Sure Boy pale kati na sijui kwanini huyu jamaa anawekwa benchi pale Yanga, hata hivyo hayo niwaachie wenyewe wana Yanga.
Nabi amefundisha jinsi ya kucheza na Waarabu ndani ya ardhi yao, alichokifanya ni kuuchukua mchezo walioucheza Club Africain hapa Dar wiki moja iliyopita na kwenda kuuhamishia kwa Yanga kule Tunisia. Zile zile mbinu za kupoteza muda walizokuwa wakizitumia Club Africain ndiyo amezitumia kwenda kuwaumiza nazo pale Tunisia.
Mara zote nimekuwa nikisema kuwa mimi ni muumini wa soka la kasi, wachezaji wanatakiwa wakimbie muda wote, wakiwa na mpira au wasipokuwa na mpira. Timu yangu ya Simba ina la kujifunza kutoka kwa Yanga na naamini kuwa kama Simba isipobadili aina ya soka la kobe (polepole) inalolicheza basi Yanga wana muda mrefu sana wa kutawala Ligi Kuu ya NBC hapa Tanzania.
Yanga siyo kwamba wana wachezaji wenye vipaji sana kuliko Simba. Yanga wana wachezaji wanaocheza soka la kisasa, soka la kasi kitendo kinachofanya mpira kuwa na 'actions' nyingi ndani ya dakika 90.
Simba tuna kawaida ya kucheza soka la taratibu sana, napenda kuliita soka la kizamani kutokana na aina ya wachezaji mafaza (wasiotaka kukimbia uwanjani) tuliokuwa nao, kitendo kinachowapa wapinzani wetu kujipanga katika kujilinda na kushambulia. Kwakweli hatupo 'aggressive' kama walivyo Yanga SC.
Narudisha tena pongezi kwa Kocha Nabi kwa kutumia akili kubwa ya kumuanzisha Aziz Ki benchi, nadhani hii iliwastua pia Club Africain, hawakutegemea kukutana nalo hili. Walikutana na kiungo flani pale kati aliyewapelekesha sana, naye si mwingine bali ni Sure Boy huku juu wakikutana na Feisal sehemu waliyotegemea wangemkuta Aziz Ki.
Nabi anajua kupanga mabadiliko yenye athari, alimuingiza Aziz Ki kipindi ambacho waarabu wamechanganyikiwa kwa kuona muda unakwenda, huku hawapati walichokuwa wakikitaka nacho ni ushindi. Aziz Ki akawafunga mdomo ndani ya ardhi ya Tunis.
Mwisho napeleka wito wangu kwa Yanga SC kuwa wasijiroge kusikiliza kelele za mashabiki kuwa wamfukuze kocha Nabi. Huyu Kocha dumuni naYe hata miaka mitano, hakika atakuja kuwafikisha mbali. Viongozi muungeni mkono kipindi cha usajili ili atoe mapendekezo yake awaletee wachezaji wa maana watakaoendana na falsafa zake.
Nimekuwa kisoka nadhani kutokana na umri kunitupa mkono kiasi ya kuwa sina ushabiki maandazi wa kukandia wapinzani wetu pindi wanapofanya vizuri. Huwa napenda kuuangalia mpira katika taswira tofauti na ya kishabiki.
Asanteni kwa kuwa nami.