Nimefurahishwa sana na ushindi wa Lissu kwenye uenyekiti wa CHADEMA. Kiukweli huu ni ushindi mkubwa sana kwa Chama Cha Mapinduzi kwa wiki hii.
Chama kimecheza karata yake vizuri kuhakikisha mtu asiye na busara wala uvumilivu wa kisiasa anakuwa mwenyekiti wa CHADEMA ili kuharakisha anguko la CHADEMA.
Imechukua miaka mingi na mbinu mbalimbali kumtoa madarakani jabali la siasa za upinzani Tanzania, Ndugu Mbowe ila ikawa ngumu. Fursa ilivyojitokeza wanaCCM tukaitumia vizuri.
WanaCCM tulijifanya tunamsapoti Mbowe ili Lissu apate kura za hasira toka kwa wajumbe wa mkutano mkuu na bahati nzuri mambo yameenda kama yalivyopangwa.
Kwa dhati kabisa ninawashukuru Ntobi na
Yericko Nyerere kwa kuhakikisha wanatoa kauli za kuwakera wajumbe na Team Lissu ili kuongeza kura za hasira kwa Lissu. Mbowe atakuwa kapata fundisho la maisha kutojihusisha na vijana wasio na nidhamu.
Kwa hapa JF nampongeza Lucas na Tlatlaah kwa kuhakikisha wajumbe wanapata hasira na kumpiga chini jabali lililotusumbua sana.